Naamini Watanzania wote tunafahamu heshima hii ya Ngorongoro Crater kama moja ya maajabu ya dunia na mtaji mkubwa sana kiuchumi kwa Nchi yetu.
Nadhani ni muda sahihi kwa Serikali kuiwezesha Mamlaka ya Hifadhi ya NgoroNgoro ili kulinda hifadhi yetu na kurejesha mahusiano mazuri ya wanyama na binadamu kama ambavyo imekuwa tangu kuanzishwa kwa hifadhi hii mwaka 1959.
Hoja ya wingi wa mifugo na zozote zingine zinajadilika kukiwa na mahusiano mazuri na wananchi na tunaiamini Serikali Mama Samia Saluhu Hassan ni sikivu.
