Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini Tanzania COSTECH, imeadhimisha siku ya Wanawake na Sayansi duniani kuwakutanisha wanawake wanaochukua masomo ya Sayansi na kujadili mambo mbalimbali ili kuongeza idadi ya wanawake wanaosoma masomo ya Sayansi katika Jamii
Akizungumza na Waandishi wa habari katika sherehe za maadhimisho hayo zilizofanyika katika Ukumbi wa Costech Jijini Dar es Salaam Afisa Utafiti Mwandamizi Kutoka tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dkt. Hulda Gideon amesema kuwa wameadhimisha siku hiyo Ikiwa ni mojawapo ya utekelezaji wa Majukumu ya Tume waliyopewa na Bunge.
"kupitia Sheria namba 7 ya mwaka 1986 kuhakikisha wanawake wanashikiriki kikamilifu katika masomo ya Sayansi huku akibainisha kuwa idadi ya Wanawake katika ushiriki wa masomo ya Sayansi haijafikia 50% ukilinganisha na wanaume"amesema Hulda
Amesema Siku hii ni muhimu sana kwa sisi wanawake na watoto wa kike na kwa kutambua muhimu huo COSTECH tumewakutanisha wanawake na wadau mbalimbali wa Sayansi ja teknolojia ili kujadili mambo mbalimbali huku lengo kubwa ni kuhakikisha idadi ya wanawake kwenye matumizi ya Sayansi na Teknolojia nchini yanaongezeka " amesema Dkt. Hulda
" Walimu wana nafasi kubwa ya kuhamasisha wanawake kuchukua masomo ya sayansi kwa kuwahamasisha na kutoa dhana ya kuwa masomo ya Sayansi ni Wanaume pekee"amesema
Kwa upande wake Dkt. Philbert luhunga kaimu Mkurugenzi Mkuu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) amesema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni kuwa wamoja zaidi na kuangalia njia mbalimbali na kushiriki katika kutatua changamoto mbalimbali za masuala ya maji na mabadiliko ya tabia ya na asilimia kubwa ya waathirika wa tabia ya nchi ni Wanawake na njia pekee ya kutatua changamoto hiyo ni mabadiliko ya Sayansi na teknolojia
