Kiongozi wa Jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amesema Jeshi litaacha kujishughulisha na Siasa baada ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2023
-
Kamati za Upinzani na Vyama vya Siasa vimekuwa vinatoa wito kwa Jeshi kuacha madaraka. Pia wamekataa maelewano yoyote yakiwemo makubaliano yaliyomrejesha Waziri Mkuu Abdalla Hamdok Madarakani
-
Kwa mujibu wa Maafisa wa Afya, takriban watu 44 wamefariki dunia katika maandamano ikidaiwa wengi wao wamepoteza maisha kwa majeraha ya kupigwa risasi
