FCC YATOA ELIMU KUHUSU USHINDANI NA UWEKEZAJI KATIKA MAONYESHO SABASABA







Na Mwandishi wetu.....

Wananchi, wawekezaji na wajasiriamali wanahimizwa kutembelea banda la Tume ya Ushindani (FCC) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ili kupata elimu muhimu kuhusu ushindani wa haki, ulinzi wa walaji, na mbinu bora za kujiimarisha kwenye soko la ndani na nje.

Kwa mujibu wa FCC, hatua hii inaunga mkono ajenda ya kitaifa ya kuvutia uwekezaji endelevu na kukuza uchumi jumuishi unaojengwa juu ya misingi ya ubora, ufanisi na usawa katika biashara.

Akizungumza katika maonesho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Juma Ngasogwa, amesema elimu wanayoitoa inalenga kuwawezesha wawekezaji na wafanyabiashara kuelewa vyema matumizi ya alama za biashara, kanuni za ushindani wa haki, na namna ya kutambua na kukabiliana na bidhaa bandia.




Ameeleza kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, FCC inalinda ushindani wa haki baina ya kampuni kwa kuzuia mbinu dhalifu au mikakati kandamizi ambayo inaweza kudhoofisha soko huru. Hii, amesema, huongeza uaminifu wa wawekezaji na kukuza ubunifu katika sekta binafsi.

Tume hiyo inasisitiza kuwa mazingira bora ya ushindani ni kichocheo muhimu cha kuimarisha tija ya kiuchumi, kuvutia mitaji kutoka ndani na nje ya nchi, na kuleta maendeleo endelevu.


"Lengo kuanzishwa tume ya ushindani ni kusimamia na kuhimarisha ufanyaji wa biashara nchini, kulinda na walaji dhidi ya mienendo potofu ya hali ya ufanyaji biashara nchini kati ya kampuni na kampuni, pamoja na kudhibiti bidhaa bandia."amesema 




Pia alisistiza kuna sheria ambayo ya kudhibiti bidhaa bandia, ni kosa la jinai kujihusisha na bidhaa bandia hivyo wananchi wafike kwenye banda la viwanda na biashara kufika ili waweze kutofautisha bidhaa bandia na halisi kwa sababu kuna wataalamu wanatoa elimu.













Previous Post Next Post