Na Lilian Ekonga.....
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeshiriki Katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara (Sabasaba) ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na madawa ya kulevya, madhara yake na mbinu za kuepukana nazo.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Afisa Elimu Jamii Mwandimizi kutoka DCEA, Said Madadi amesema Mamalaka ina mikakati muhimu minne ambapo mkakati wa kwanza ni kupunguza uzalishaji, uenezaji na usambzaji wa dawa za kulevya nchini
"Katika eneo hili zipo divisheni ambazo zinafanya kazi ya kuzuia katika mipaka, mashamba na uzalishaji wa ndani" amsema Madadi
Amesema kuwa Makakati wa pili wa Mmalaka ni kupunguza uhitaji ambapo kuna watu wanazalisha hapa ndani kwenye mashamba na dawa zingine zinapita katika mbinu za siri ambazo wanazijua wengine tayari wameshawakamata
Ameongeza kuwa katika Maonesho Wanatoa elimu Kinga ya kuwalinda jamii endapo watafikiwa na dawa hizo kwa njia zozote wajue madhara yake ambayo wameshafahamishwa kwenye Elimu wanayotoa.
Amesema Makakati wa tatu wa Mamlaka ni kupunguza hatari itokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya huku Mkakati wa nne ukiwa ni kuimarisha mahusianao na taasisi mbalimbali ili tarifa ziweze kuwafiki wananchi.