WIZARA YA KATIBA YA SHERIA MSHINDI WA KWANZA MIONGONI MWA WIZARA ZOTE ZILIZOSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA



Na lilian Ekonga....

Wizara ya katiba na Sheria imepokea tuzo ya Mshindi wa Kwanza miongoni mwa wizara zote zilizo shiriki katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendeles katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam.

Tuzo hiyo imetolewa leo na Rais wa Serikali ya Zanzibar, Mhe Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati ufunguzi ramsi ws maonyesho hayo.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula amewapongeza watumishi Kwa jitahada zao pamoja na huduma walizozitoa zimewavutis wananchi wengi katika kutoa msaada wa sheria na Elimu kuhusu Katiba.

Haya ni maonssho ya biashara kwenye biashara kuna vitu vitatu lazima uvipate, moja ni katiba ambayo ni sheria mama na chapili ni sheria maana kuna mikataba" amessma Dkt . Rwezimula

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria Mkurugenzi Msaidizi Bi. Beatrice Mpembo amesema wanashukuru viongozi wao kwa kuwa bega bega nao pale wanapo wanapohitaji msaada na wamehaidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii.







Previous Post Next Post