WCF IMEWALIPA FIDIA WAFANYAKAZI 19650 WALIOPATA CHANGAMOTO KAZINI




Na Lilian Ekonga.....

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi umefanikiwa kuwalipa fidia wafanyakazi na wategemezi wao wapatano 19,650 waliopata ajali,kuugua au kufariki kutokana na Kazi.

Ameyasema hayo leo May 15, jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma wakati akizungumzia mafanikio WCF ambayo yamepataikana ndani ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake.


Mduma amesema mafanikio mengine ambayo wameyapata ni kuongeza mafao saba makuu ambayo ni pamoja na fao la ulemavu wa kudumu, fao pensheni kwa wategemezi, fao la wasaidizi wa mgojwa , fao la utengamano na fao la msaad wa mazishi.

Ameongeza kuwa mafanikio mengine ambayo WCF wameyapata ni ubirsshaji wa mifumo ya TEHAMA,mfuko huo hivi sasa umetekeleza mapinduzi ya kidigital8 kwa zaid ya 90% ambapo huduma zote zinapatikana kwa njia ya Mtandandao

"Vilevile mfuko umeendelea na kampeni mbalimbali za elimu na uhamsishaji kwa waajiri na wafanyakazi juu ya haki zao, taratibu za fidia na usalama mahali pa kazi, Elimu hii imesaidia kupunguza ajali na magojwa kazini, pamoha na kuongeza usajili wa waajiri," amessma Dkt. Mduma



Mbali na mafanikio hayo, Dkt. Mduma amesema Juni, mwaka 2024 WCF ilipata cheti cha, ithibati cha ISO (ISO Certification) kwa utoaji wa huduna bora kwa viwango vya Kimataifa, jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa mfuko huo kuwapa matumaini wadau wao.

Pia, mwaka 2023 mfuko huo ulipata tuzo ya ISSA (International Social Security Association) kwa matumizi bora ya TEHAMA na mwaka huu 2025, WCF ilishika nafasi ya pili katika tuzo za eGA na nafasi ya tatu kwenye Tuzo za TEHAMA 2025 kwa taasisi za umma zilizofanikiwa kuondoa urasimu kupitia TEHAMA.



Hata hivyo, mbali na mafanikio hayo, Dkt. Mduma amesema, wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo wanaendelea kuzifanyia kazi ikiwemo waajiri kutosajili na kuwasilisha michango kwa wakati.

"Baadhi ya waajiri bado hawajatekeleza matakwa ya sheria ya kuwasajili wafanyakazi na kuwasilisha michango kila mwezi. Hili linawanyima haki wafanyakazi wanapopatwa na majanga kazini," amesema

Mkurugenzi huyo wa WCF amesema licha ya changamoto hizo mfuko huo umeendelea kujidhihirisha kuwa ni chombo muhimu cha ulibzia wa kijamii kwa wafanyakazi nchini.

Aidha, WCF umekuwa mfano wa kuigwa barani Afrika, na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wamezishauri nchi mbalimbali kujifunza jinsi unavyoendeshwa na alizitaja nchi ambazo zimefika nchini ni pamoja na Kenya, Zambia, Malawi na Ethiopia.

"Eswatini tuna miadi nao, wanataka kuja kujifunza, Afrika Kusini tulibadilishana nao uzoefu maana wao wana miaka 20 katika kuwalipa fidia wafanyakazi, walitushauri kutumia Akili mnemba (Artificial Intelligence), nasisi wamejifunza kumtambua mwajiriwa na mwajiri, wao kwasasa wanamtumua mwajiri," amesema

Dkt. Kaduma kupitia mkutano huo alisisitiza kuwa, wataendelea kuboresha huduma, kushirikiana na wadau wote na kuhakikisha wanasimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi ili kila mfanyakazi anapopatwa na madhira anapata haki yake kwa wakati.

"Natoa wito kwa waajiri wote kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na kwa wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, wakijua kuwa mfuko wao uko imara na thabiti kuwahudumia," alisisitiza Dkt. Mduma.





Previous Post Next Post