Katibu tawala Mkoa wa Dar es salaam Dkt Toba Nguvila ameitaka Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa umma –PPRA kuwasajili katika mfumo wa Nest makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu ili kushiriki katika ukuaji wa uchumi.
Ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati akifunga mafunzo kwa jumuiya ya wasioona Tanzania -TAB hafla iliyoambatana na ugawaji wa vifaa saidizi vya mafunzo iliyoandaliwa na Mamlaka ya udhibiti wa ununuzi wa Umma -PPRA.
Amesema kusajiliwa katika mfumo wa Nest itasaidia kufikiwa na fursa mbalimbali ambazo Serikali imeendelea kuzitoa ikiwemo mikopo na mafunzo.
Awali akiongea Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema msaada huo utawasaidia kwa walemavu kuchangamkia fursa kwenye ununuzi wa Umma zinazotangazwa kwenye mfumo wa Nest.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Umma (PPRA) Dennis Simba amesema mafunzo kwa kundi ya watu wasiona yamegharibu milioni 52 kwa mkoa wa Pwani kwa washiriki 250 huku wakitoa redio na memorikadi hivyo waliona muamko kwa walemavu ni mdogo hivyo wanaweka mkazo kwa makundi hayo na wao wanapaza hizo kazi.
Nae Mwenyekiti wa jumuiya cha Wasiona Tanzania -TAB Omary Kitangu amesema redio hizo na memori walizopewa zitawasaidia kujua tenda za serikali zilizowekwa kwa walemavu kwa asilimia 30 na zitawasaidia kuwanufaisha walemavu.
Alikadhalika ameiomba mamlaka hiyo kutanua mafunzo yake katika mikoa mingine ikiwemo Kusinini hasa Mtwara na Lindi.
Mpango wa Serikali kwa sasa ni kuhakisha inaongeza ushiriki kwa makundi maalum ikiwemo watu wenye ulemavu ili kupunguza ombwe la utegemezi kwenye jamii kama vile kuwa omba