MWENYEKITI Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile amewataka waandishi wa habari kuchukua tahadhari na kutanguliza mbele usalama wao hasa katika kipindi cha kuripoti matukio yenye vunguru .
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu matukio yaliyotokea katika Mahakama ya Hakimu ya Kisutu katika kuripoti habari za Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Balile amesema waandishi wa habari wanatakiwa kuwa na jaketi na vitambulisho na kufata utaratibu wa kitaaluma unaotakiwa.
"Tulifanya utaratibu wa kukutana na jeshi la polisi tulizungumza na kamanda Murilo kwamba kuwazuia waandishi kuingia Kisutu sio jambo jema kwani hawaendi kumpigia debe mtu yoyote wanaenda kujulisha umma kuwa kuna hiki na kile kimetokea.
Balile amesema wamekubaliana na polisi kuwa waandishi wote wataruhusiwa kuingia kwenye viwanja vya mahakama ya Kisutu tarehe 6 kwenye kesi ya Tundu Lissu. "Lazima watambulike kwanza kuna jaketi hii inasaidia polisi kutambua kwa haraka kwamba huyu ni Mwandishi imendikwa press hata vitani ukiangalia kinachowatambulisha ni helement na jaketi,pili ni kitambulisho na press card tujitahidi sana kila sehemu tuwe na kitambulisho na sio kuonesha kifaa chako.
Aidha amewataka waandishi wa habari wanaokubwa na changamoto mbalimbali katika kuripoti habari watoe taarifa kwa jukwaa hilo.