Na Lilian Ekonga.....
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolfu Mkenda amewataka waandishi wa vitabu kuwa wabunifu katika Uandishi wao ili vitabu vyao viweze kuingizwa kwenye mitaala ya Elimu nchini.
Profesa Mkenda amebainisha hayo leo Aprili 07 Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wandishinwa habari kueleke kilele cha utoaji tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo itafanyika aprili 13 kwenye ukumbi wa super dom masaki.
Amesema Tuzo hizo zinalenga kukuza lugha ya Kiswahili na kuongeza ufanisi katika matumizi ya lugha hiyo na kuinua Waandishi Bunifu.
Prof. Mkenda amesema mbali na Tuzo hizo kukuza lugha la kiswahili lakini pia Tuzo hiyo inalenga kuendelea kuenzi Mchango wa Baba wa Taifa katika Taifa la Tanzania.
"Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha utoaji wa tuzo hizo zinazotarajiwa kutolewa April 17, 2025" amesema Prof Mkenda
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt Aneth Komba amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020 umeendelea kuwa na Mafaniko makubwa ikiwemo kuwainua waandishi Bunifu wa Tanzania.
Naye wake Mwenyekiti wa Tuzo ya Taifa ya Mwl. Nyererewa Prof. Penina Mrama ameeleza idadi ya watu Watakao wania tuzo hiyo katika Vipengele vinne na zawadi zitakazo tolewa kwa Mshindi wa kwanza hadi wa tatu.
"Utaratibu wa zawadi kwa washindi utabaki kama ilivyokuwa miaka iliyopita yaani, Mshindi wa kwanza Shilingi milioni 10, Muswada wake utachapishwa na serikali na kusambazwa shuleni na maktaba za taifa, Ngao na Cheti. Mshindi wa Pili atapata Shilingi milioni 7 na Cheti, pia Mshindi wa tatu nae atapata Shilingi milioni 5 na Cheti". Ameeleza Prof. Mlama.