TUWEKEZE NGUVU KWENYE UWEZESHAJI WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA UONGOZI-WAZIRI GWAJIMA





Na mwandishi wetu....

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Gwajima, amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana ili kufanikisha ustahimilivu wa kiuchumi, kushinda changamoto, na kuishi kwa heshima.

Akizungumza katika hafla ya kusherehekea mafanikio ya uongozi wa wanawake vijana nchini Tanzania, iliyoandaliwa na shirika la Her Initiative linalowawezesha na kuwaunga mkono wanawake vijana na wasichana katika kufikia ustahimilivu wa kiuchumi, kushinda vikwazo, na kuishi kwa heshima, Waziri Gwajima alimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kama kielelezo cha mafanikio ya uongozi wa wanawake na msukumo kwa mabinti na wanawake kote nchini.

Waziri Gwajima alieleza mafanikio ya Tanzania katika kuongeza uwakilishi wa wanawake bungeni kutoka asilimia 8% mwaka 1995 hadi 37% mwaka 2020, huku akisisitiza dhamira ya serikali katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia mikopo nafuu na fursa za elimu bora.




*"Tunapaswa kuunda utamaduni unaowawezesha wasichana na wanawake vijana kufanikisha ndoto zao na kuishi kwa heshima,"* alisema Waziri Gwajima.

Aidha, Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania, Peter Huyghebaert, amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji ni mzuri katika kuhakikisha wanawake na mabinti wanapata fursa sawa katika nyanja zote.

"Usawa wa kijinsia ni jambo la msingi kwa maendeleo ya jamii. Tanzania na Ubelgiji zimeshikamana kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa katika elimu, ajira na uongozi. Tunashirikiana katika miradi mbalimbali kama Wizeka Binti, Empower the Girl, na Binti Digitale kuhakikisha kila msichana anaweza kutimiza ndoto zake," alisema Balozi Huyghebaert.

Mkurugenzi Mtendaji wa Her Initiative, Lidya Charles, amemshukuru na kumpongeza Waziri Dkt. Gwajima kwa kuwa kiongozi imara na kwa juhudi zake za kupambania ndoto za vijana wa kike na wa kiume kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii.




"Shughuli hiyo imekuka baaada ya shirika lao kutapa tuzo mbili mwaka jana kupata tuzo mbili za kimataifa zilizopelekea kusheria tukio hilo na kutengeza mazingira kwa vijana na wasichana wa kitanzania kufahamika kimataifa na kazi zao wanazozifanya ziweze kujulikana." Amesema Moyo


Pia amemshukuru Waziri Gwajima kwa kumteua Kutengeneza kamati na kuweza kutengeneza tamasha litakayozungumzia vitu tofaut ambavyo tutavifanya kuhakikisha kwamba kazi zinazofanywa na wasichana wizara inafahamu na jinsi gani wataweza kushirikisha wadau wengine ili kazi wasichana na vijana kuwa na nguvu zaidi.

Adiha akizungumzia maadhimisho ya miaka 30 ya Beijing Lydia amesema kupitia beijing imeweza kuwakuza wanawake na wasichana kama nchini kwetu tumeweza kuwa na Rais Mwanamke na tumeona wanawake wengi wakishiriki katika Uongozi mbalimbali hasa katika miuondombinu, Afya na Elimu.





Previous Post Next Post