SERIKALI YATENGA BILIONI 28 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA CHINI.

 




Serikali ya  Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya  Awamu ya sita imetenga kiasi cha fedha cha Bilioni 28 ili kwenda kuboresha miundombinu ya barabara Nchini kupitia wakala wa barabara mijini na Vijijini (TARURA).


Akizungumza kwenye mafunzo yaliyofanyika  jijini Dar es salaam Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa tarura  Mhandisi Ismaily Mafita amesema kuwa 

Semina hii ya wakala wa vijijini na mijini (TARURA)Tumeweza kutoa  elimu ya ujenzi wa madaraja na barabara  kwa wanahabari wa mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) ili kwenda  kutoa uwezo wa kutoa habari kwa jamii.


Lengo ni kuwapatia elimu wananchi kuhusu miundombinu ya barabara ambapo kuna baadhi ya njia zinatumiwa na magari makubwa na kupelekea uharibifu wa njia hizo.


"Kupitia semina hii tarura tunategemea kuwa barabara zote Nchini ni muhimu kwa matumizi ya watu lakini njia ya barabara ndio inatumika kwa asilimia 80 inatumiwa kwa usafirishaji na usafiri."Alisema Mhandisi Mafita. "


Barabara zina mchango muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuendesha maisha yao  kwani bidhaa nyingi zinasafirisha bidhaa kupitia barabara.



Wakala wa mijini na vijijini tarura wameweka zaidi ya kilomita 5000 kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo mkoa wa Dar es laaam.


Hata hivyo wakala wa miji na vijijini (TARURA) wanaendelea na kutumia teknolojia mbadala katika kujenga madaraja ya mawe na kuongeza wigo wa ajira Nchini kwa vijana ambao hawana ujuzi.


Aidha  tuna miradi ambayo inafadhiliwa na benki ya dunia ambayo inatekeleza Mradi wa DMDP awamu ya pili ambapo unaenda kuendesha ujenzi wa miundombinu ya barabara dar e salaam na mifereji ya Mvua. 



Katika hatua nyingine kiasi cha fedha  shilingi Milioni 28.5  zinaenda kutumika katika halimashauri zote tano za mkoa wa dar es salaam hivyo wanahabari wa mitandao ya kijamii nendeni mkahabarishe umma suala hili muhimu ambalo linahusu ujenzi wa miundombinu,  barabara na mifereji.



Kwa upande wake  Dkt Heladius  Makene  kutoka kitengo cha mazingira na jamii ameongeza kuwa tunamshukuru  Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt samia suluhu Hassani kwa kuweza kuona barabara za mijini na vijijini  TARURA na kutuwezesha  kutoa fedha ambazo zimewezesha kujenga barabara zetu.





Naye  Mhandisi  Pharles Ngeleja    ambaye anatengeneza madaraja ya mawe  amesema kuwa mwaka 2024 barabara zetu zimefikia kiasi kadhaa ikiwa ni kilomita 3000 huku serikali ikiendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara zote zikiwemo Mjini, na Vijijini. Ambazo ni barabara za lami, na zege.



Mhandisi Ngeleja ameongeza kuwa kuna baadhi ya barabara zimeongezeka hivi karibuni huku baadhi ya changamoto zinaendelea kutatuliwa na serikali yetu na mabadiliko ya tabia ya nchi ikichangia katika kutengeneza barabara zetu hivyo kupitia Tarura tunatumia vifaa ambavyo vinapatikana Kwenye maeneo hayo  ambapo  tunajenga barabara na madaraja."Amesema Mhandisi Ngeleja"



Vilevile   Makamu Mwenyekiti kutoka jumuiya ya   Mitandao ya kijamii Tanzania (JUMIKITA) Humphrey shayo  amesema kuwa sisi kama wanahabari wa mitandao ya kijamii JUMIKITA tunahabarisha umma kwa muda mfupi hivyo tunaipongeza Tarura kwa kutambua mchango wetu wa kuhabarisha jamii kutoka sehemu moja kwenda nyingine



Previous Post Next Post