Ameyasema hayo leo alipongea na waandishi wa Habari kuhusiana na maandalizi ya Tamasha hilo. “Maandalizi ya tamasha yanaendelea vizuri na tunakaribisha wadhamini kuja kusaidia kufanikisha Tamasha hili kubwa ambalo litafanyika Mikoa yote ya nchi yetu ya Tanzania tukianzia na Mkoa wa Dar es Salaam.
Ndugu Alex Msama Mwenyekiti wa Kamati ya Mandalizi ya tamasha hilo amesema kwasasa jambo kubwa linalofanyika ni kuendelea kuzungumza na wafadhili na tukifanikiwa tu kupata wadhamini basi tamasha litakuwa halina kingilio litakuwa bule.
Tamasha la Kuombea uchaguzi litafanyika hivi karibuni na kuwaunganisha waimbaji mbali mbali wa nyimbo za injili Ndani na Nje ya Tanzania.