"NAOMBA MNÄ°KUMBUKE KWENYE MAOMBI YENU" MSAMA




Mkurigenzi wa Msama Promotion Alex Msama awaomba waumini wa kanisa la Reconciliation missionary Babtism lililopo Kigamboni Dar es salaam kuzidi kumuombea.

Msama ameyasema hayo leo March 15,2025 alipoalikwa kama Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa kanisa hilo.

“Niwaombe ndugu zangu wa Kristo msiache kujitoa kwa Mungu hata mimi hapa mnapo niona yapo mengi napitia katika Biashara zangu lakini Sadaka zinanisaidia mimi kuendelea kuwa Imara niwaombe tu mnikumbuke katika maombi yenu.

Katika hafla hiyo Msama ameahidi kuchangia ujenzi wa kanisa hilo upande wa Malumalu za kanisa pamoja na Gipsum ili kuendelea kulisapoti kanisa hilo kwenye upande wa ujenzi.
Previous Post Next Post