Na lilian Ekonga......
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema zoezi la kuwarejesha wafanyabiashara kwenye soko la Kariakoo lililopata ajali ya moto Julai 10, 2021 na kusababisha wafanyabiashara hao kuondolewa na shughuli kusimama, linatarajiwa kuanza mapema Februari mwaka huu huk
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Januari 29, 2025 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Masoko ya Kariakoo Hawa Ghasia amesema hatua hiyo ni kufuatia uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo, baada ya kukamilika kwa ujenzi na ukarabati wa soko, sambamba na kukamilika kwa kazi ya uhakiki wa waliokuwa wafanyabiashara kwenye soko hilo, uliofanywa na Timu Maalum iliyoundwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ikijumuisha wawakilishi wa Wafanyabiashara, Menejimenti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na vyomba vya Usalama.
Amesema kuwa Menejimenti inaratibu kazi ya kutangaza majina ya waliokuwa wafanyabiashara kwenye Soko hilo ambao wamekidhi vigezo na sifa za kurejeshwa baada ya uhakiki, ambapo Uhakiki uliofanywa umebaini jumla ya wafanyabiashara1,520 wanaotarajiwa kurejeshwa sokoni, huku Majina na fomu ya kujiunga yakitarajiwa kwa umma kupitia vyombo vya habari ikiwemo tovuti ya Shirika la Masoko ya Kariakoo na tovuti ya OR - TAMISEMI.
"Kuna fomu ya kujiunga tutairusha kwenye tovuti hizo kwa wale ambao wafanyabiashara wanastahili kurejewa watatkiwa kujaza fomu na kupewa utaratibu wa kurejea" amesema Ghasia
Aidha, Bi. Hawa Ghasia ametoa wito kwa Wafanyabiashara wote wenye madeni ya awali kabla ya soko hilo kuungua kulipa madeni yao kabla ya kurejea Sokoni, huku akieleza kuwa takwimu zinaonyesha takribani wafanyabiashara 366 wanadaiwa na Shirika hilo jumla ya Shilingi 358,571,106.85.
Soko hilo ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni 28.03 zilizotumika kufanikisha mradi wa kimkakati wenye nia ya kulifanya Soko la Kariakoo kuwa la kimataifa, mradi ambao ujenzi na ukarabati wake ulianza Januari 2022