Na Lilian Ekonga.....
Rai hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi wa bandari ya dar es salaam Abedi Gallus wakati wa ziara ya jumuiya ya wafanyabiashara taifa jwt kujionea utendaji wa bandari hiyo ambapo amesema kwa sasa muda wa kuhudumia shehena umepungua kutoka siku 10 na kufikia wastani wa siku tatu.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2023 mamlaka ya usimamaizi wa bandari tanzania iliweza kuwashirikisha wawekezaji wawili katika bandari ya dar es salaam, Adan ports na Dp World ambao wanafanyakazi pamoja katika bandari ya Dar es salaam.
"Ujio wa wawekezaji hawa umeleta mabadiliko makubwa katika utendaji ambapo muda wa meli wa kupakua mizigo umepungua kuliko apo awali meli zilikuwa zinasubiri zaidi ya siku 30 nje lakina kwa sasa meli za makasha zinafunga moja kwa moja pale zinapofika"amesema
Ameongeza kuwa muda wa kuhudumia shehena zikiwa ganitini zimepungua ambapo apo awali tulikuwa tunahudumia meli7 zaid ya siku 10 na kwa sasa tunahudumia shehena ya makasha kwa wastani kwa siku tatu ambapo zimeleta matokeo chana kwa wafanyabiashara na kutembelea bandari ya dar es salaam kujionea kinachoendelea.
Aidha amesema meli ambayo iliyokuwa inashusha kontena kwa siku kumi itashusha kwa siku tatu na wakiongeza hiyo mashine nyingine itapelekea meli ilitokuwa inashusha kws siku 10 kususha kwa siku tatu au siku moja.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara taifa Hamisi Livembe amesema maboresho yaliyofanyika bandarini hapo yameharakisha ufanyaji wa biashara nchini na hivyo kuongeza vipato vya wafanyabiashara na taifa kwa ujumla.
"Kuna mbadiliko makubwa yamejitokeza na bado yanaendelea3 na uwekezaji kama tunavyoona kuna mashine kubwa zimekuja kufanya ufanisi kwa utoaji mizigo na kulikuwa na mashine mbili na wanaleta nyingine ya tatu na hizi mbili hizi mashine mbilu zilikuwa zinashusha kontena 1000 kwa siku amesema
Naye Elitunu Mallamia ambaye ni meneja mahusiano wa kampuni ya DP wolrd amesema kwa kipindi kwa mwezi disemba 2024 wamefanikiwa kuhudumia meli 16 na magari takribani 25251 hivyo wanaendelea kuboresha miundombinu ili kuongeza ufanisi.