MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo, kuhusu maandalizi ya bonanza la mwezi wa mlipakodi la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Meneja TRA Mkoa wa Kodi wa Kariakoo, Kabula Mwemezi na kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Seleman.
Katibu Tawala Wilaya ya Ilala, Charangwa Seleman, akizungumza na wafanyabiashara wa Kariakoo, kuhusu maandalizi ya bonanza la mwezi wa mlipakodi la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jijini Dar es Salaam.
Meneja TRA Mkoa wa Kodi wa Kariakoo, Kabula Mwemezi, akizungumza na wafanyabiasha hao.
Na lilian Ekonga..............
Kuelekea kilele cha wiki ya mlipa kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imeandaa bonaza kwa wafanyabishara wa karikoo litakalo jumuisha michezo mbalimbali ikiwemo kutembea kwa kilometa 5 kwa wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa TRA.
Ameyasema hayo leo januari 16, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo wakati akazingumza na wafanyabiashara wa w akarikoo ambapo amesem bonaza hilo litafanyika januari 19,2025 katika viwanja vya kidongo chekundu jijini Dar es salaam.
"Kutakuwa na michezo ya kukimbiza kuku, michezo ya kuvuta kamba kati jumuiya ya wafanyabiashara , kukimbiza yai kukimbia na magunia kila michezo itakuwepo pale" ameseama Dc mpogolo
Alikalika amesema baada ya bonaza hilo kamshina Mkui wa TRA, Yusuph Mwenda ataenda kuzungumza na wafanyabiashara wa kariakoo kwa lengo la kusikiliza changamoto na kupokea maoni mbalimbali.
Aidha amewasisitiza wafanyabiashara wote wa kariakoo kuweza kushiriki kwenye bonaza na kalbu za joging za kariakoo kuweza kuahiriki bonaza hilo la TRA ili waweze kuonyesha ushirikianao wao kwao.
Kwa upande Mwenyekiti wa Umoja wa wafanyabiashara kariakoo, Severian Mushi ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA na Kamshina Mkuu wa TRA kwa kuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero zao na utendaji mzuri kati ya makamishina na wafanyabiashara wa kariakoo.
"Tunashukuru kwa kuchagua kariakoo kuwa kilele cha mlipa kwa kuandaa bonanza hili na sisi tupo tayari kwa bonaza hilo na tumeandaa kwa mda mfupi kutoka mambo yaliyo nje ya uwezo wetu" amesema Mushi