Na Mwandishi wetu..Dar es salaam
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emanuel Tutuba ametoa wito kwa Wafanyabiashara na wananchi nchini wanaopata fursa ya mikopo ya serikali na kurejesha kwa wakati na watumie fedha vizuri na wasidhani kuwa ni zawadi kutoka serikalini
Wito huo ameutoa leo Januari 31, 2025 wakati wa kikao kilichowakutanisha BoT, Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Kampuni ya Airpay Tanzania, wadau kutoka Taasisi za kibenki na mitandao ya simu.
Amesema fedha hizo ni za uwezeshaji wananchi kiuchumi ambapo lengo lake ni kuwajengea fursa ya kuwa na shughuli za kiuchumi zinazotengeneza faida.
"Na sisi kama wasimamizi wa sekta tunaendelea kuweka mifumo vizuri ya kuhakikisha serikali inawawezesha wananchi na wananchi wanafanya biashara zao wanapata faida na wanarejesha na kuendelea na biashara zao." Amesema Tutuba
Ameeleza kuwa viongozi wa serikali wamekuwa wakisisitiza kila mwenye vigezo vyote akope mkopo na arejeshe lakini kila anayepata fursa ajue kwamba amebahatika kwa sababu serikali imeweka mifumo ya kuweza kurejesha fedha hizo kwani angeweza kupata kwa gharama kubwa.
"Utaratibu wa kurejesha ni mzuri kwa mtu ambaye atakuwa anarejesha ili iweze kujenga matumaini kwa wananchi wengine kwa kurejesha kwa wakati." Amesema
Akielezea namna mikopo ambavyo imekuwa hairejeshwi, Tutuba amesema kiwango cha mikopo chechefu kimekua kwa wastani wa asilimia 28 ya mikopo ambayo hairejeshwi bila kuwa na sababu za msingi.
Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi Zanzibar (ZEEA), Juma Barhan Mohamed amesema kuwa kikao hicho kimewasaidi kuwa na mpango wa pamoja na wadau wote wa fedha kidijitali.
Hata hivyo Juma alisema anaishukuru kampuni ya Airtel na Benki ya TCB kuwa kampuni za kwanza za kifedha kuweza kukamilisha muunganisho wa mifumo ya malipo kidijitali na ZEEA pamoja na Airpay.
“Hichi kilichofanywa na kampuni hizi mbili kimesaidia na kimeonesha jinsi gani wanaunga mkono serikali katika kuhakikisha tunakuwa na uchumi jumuishi visiwani Zanzibar,”
Tunaamini baada ya kikao hiki cha leo wale ambao hawafanyi marejesho watarejesha kiurahisi zaidi bila ya kuwa na kikwazo cha kusafiri kutoka sehemu moja ama nyingine kwaajili ya kurudisha marejesho kwa wakati." Amesema
"Sisi kama wawezeshaji wa wananchi kiuchumi tunajukumu la kuhakikisha wanaubadilisha uchumi wa kawaisa na kwenda uchumi wa kidijitali." Amesema Mohamed
Amesema kuwa kumekuwa na nadhria mbaya kuhusiana na pesa ya serikali kwamba watu wasirudishe licha ya 0kufanya kazi vizuri na mabenki sasa pesa zinarudishwa baada ya kufanikiwa kufanya kazi na benki na tafiti mbalimbali, kwamba wasiofanya marejesho kwa wakati sio wafanyabiashara, biashara wanazo ila wamekuwa na mtazamo wa fedha ya serikali, hairudishwi rejesho.
Amesema kuwa wanaokopa watakuwa na fursa ya kurejesha kidijitali akiwa mahali popote huku nauli na usumbufu mwingine ukawa ni sehemu ya marejesho ya mkopo.
Kwa Upande wa Ofisa wa Mifumo kutoka Airpay, Mihayo Lumo amesema kuwa kwa upande wa Zanzibar tayari kuna mifumo mbalimbali kwa kila benki na mitandao ya simu wanachotaka ni kuunganisha mifumo hiyo pamoja ili iweze kumrahisishia wananchi na wananchi kulipa kwa mikopo ya ZEEA.
"Sisi kama ZEEA tumejenga mifumo wa 'Loan Management system' ambayo ni kama chungu cha mifumo yote ya ZEEA itakayokuwa inawasaidia wananchi kulipa marejesho yake kwa kwenda kwa wakala yeyote kulipa ." Amesema Lumo.
Akielezea Changamoto wanayoipitia amesema kuwa kunabaadhi ya wananchi wanakuwa hawataki tuu kutoa marejesho na kufanya mkopo kuwa Chechefu.