Na Mwandishi wetu dar....
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetakiwa kuimarisha matumizi ya teknolojia, na kuhakikisha kwa kiasi kikubwa inafanya shughuli zake kidigitali ili kwenda sambamba na kasi ya ukuaji wa teknolojia hapa nchini na Duniani kote kwa ujumla wake
Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Fedha nchini Hamad Hassan Chande wakati wa hafla ya uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa 'Soko la Bima Tanzania' kwa mwaka 2023, hafla iliyofanyika leo, Ijumaa Novemba 22.2024 kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema sekta ya bima inayo jukumu kubwa na la msingi la kuhakikisha inasaidia kujenga uchumi imara na kuwapa wananchi ulinzi imara wa afya zao
Katika eneo hilo, Chande aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo amesema hivi karibuni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya 'Bima ya Afya' kwa wote ambayo kwa namna moja au nyingine inalenga kuona kila Mtanzania anakuwa na 'Bima ya Afya' hatua ambayo ameitaja kuwa ni kubwa na inayopaswa kuchangamkiwa na kila mmoja
Aidha, Chande amebainisha kuwa tafiti na tathmini mbalimbali zinaonesha kuwa soko la bima limekuwa likipanuka kukua kila siku na kwamba kwa taswira ya uzinduzi wa mwaka huu inaonesha wazi kuwa soko hilo litaendelea kukua zaidi hivyo ni wakati muafaka sasa kwa TIRA kujipanga kikamilifu na kuhakikisha inaenda sambamba na ukuaji wa soko
TIRA pia imetakiwa kusimama mstari wa mbele na kuhamasisha uwekezaji, sambamba na kuhakikisha sekta ya bima inaendelea kuimarika maradufu
Hiyo, kwa mujibu wa Naibu Waziri Chande amesema inapaswa kwenda sambamba na mamlaka hiyo kugeukia fursa za bima zilizopo kwenye sekta ya michezo nchini, sekta ambayo ameitaja kuwa inakua kwa kasi hivyo ni vyema ukafanyika utafiti ili kuona namna bora ya kuwafikia wadau wa michezo kwa ujumla wake
Ametumia nafasi hiyo, kutoa pongezi kwa Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) na Benki ya Biashara ya NBC ambao ni wadhamini wakuu wa ligi kuu soka Tanzania Bara (NBC Premiere League) kwa kuanzisha mchakato wa mazungumzo na baadhi ya makampuni ya bima na kuingianao mikataba na kampuni hizo
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na sekta binafsi akiwemo Mwenyekiti wa Mabalozi wa Bima Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Saidi, Waziri wa zamani wa Kilimo nchini ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM) na Balozi wa Bima Tanzania Japhet Hasunga nk
TIRA pia imetumia hafla hiyo kutoa tuzo kwa wadau na taasisi mbalimbali wanazofanyanao kazi kwa karibu au zinazofanya kazi zinazohusu bima na kutoa ushirikiano wa karibu kwao ikiwemo TRA, Jeshi la Polisi, Ofisi ya DPP, wanahabari, Mabalozi wa Bima nk.
Na Mwandishi wetu dar.......