Na Lilian Ekonga Dar.......
Serikali kupitia wizara ya Fedha imekitaka chuo cha kodi (ITA) kufanya tafiti ambazo zitatatua changamoto katika mfumo wa forodha na kodi nchini na kujenga mfumo bora wa kodi ambao utarahisisha ulipaji wa kodi kwa hiyari.
Hayo ameyasema leo jijini dar es salaam Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Elijah Mwandumbya akimwakilisha Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba kwenye Mahafali ya kumi na saba kwenye chuo cha kodi (ITA) ambapo wamehitimu jumla ya wahitimu 417.
Elijah amesema Chuo kijikite na tafitia ambazo zitatoa suluhu za changamoto kwenye mfumo wa ukusanyaji wa kodi huku mapendekezo mengi kwenye tafiti yanakosa utafiti kwenye jamii hivyo yataleta mapendekezo na tafiti kwenye kufikia malengo wanayoyataka.
Aidha Elijah Amewasisitiza Chuo kiendelee kutoa mafunzo ya viwango vya juu kuzingatia kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani ndipo dunia inapoelekea kwa sasa.
"Ni wito wa mheshimiwa waziri kuona kwamba chuo hiki kinatumika vizuri zaidi kwenye kuleta tafiti zitakazo tupeleka kwenye kufikia malengo" amesema elijah
Awali akiongea Prof.Isaya Jairo Mkuu wa Chuo cha Kodi Mamlaka ya mapato Tanzania (ITA) amesema Chuo kimetengeneza wataalamu wengi wa forodha ya kodi yenye misingi ya kujenga umahiri kwenye kukuza uchumi wa Taifa pamoja na kutumia fursa za uendeshaji wa teknolojia na sayansi wa sasa ambapo itawasaidia wahitimu hao waendane na kasi ya teknolojia na forodha ya dunia ya sasa.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Kodi Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda amesema baraza lililopo liendelee kufanya kazi ili kufanikisha watumishi ambapo itawezesha kuongeza idadi ya walipa kodi pamoja na kuongeza ulipaji kodi kwa nchi na wataendelea kuboresha miundombinu ili watoe wahitimu bora kwa maendeleo ya nchi.
Chuo hicho kimetunuku vyeti kwa wahitimu 417 wa kozi mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2023/2024 huku idadi hiyo wanaume ni 236 na wanawake 181 ambapo195 wametunukiwa cheti cha Uwakala wa forodha wa Afrika Mashariki(EACFF),Wahitimu 28 wametunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM),
61 wametunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na kodi (DCTM), 119 wametunukiwa Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na Wahitimu 14 wametunukiwa Stashahada ya Uzamili katika Kodi (PGDT).