BOT YAFUNGIA APPS 69 ZINAZOTOA MKOPO MTANDAONI.








Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuwa imebaini kuwepo kwa Majukwaa na Programu Tumizi'Applications" zinazojihusisha na utoaji wa mikopo kidijitali bila ya kuwa na leseni na idhini kutoka Benki Kuu ya
Tanzania.

Aidha, Majukwaa na Programu hizo zimeshindwa kukidhi matakwa ya Mwongozo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha wa Daraja la Pili wanaotoa huduma za mikopo kwa njia ya kidijitali wa mwaka 2024uliotolewa na Benki Kuu tarehe 27 Agosti, 2024 (Guidance Note on Digital Lenders Under Tier 2 Microfinance Service Providers, 2024)





Mwongozo huo unalenga kuimarisha usimamizi wa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili nchini na kuhakikisha uzingatiwaji wa Kanuni za Kumlinda Mlaji wa Hudumaza Fedha,ikijumuisha uwazi, uwekaji wa tozo na riba, njia za ukusanyaji wa madeni, nautunzaji wa taarifa binafsi za wateja na kulinda faragha zao.

Kupitia taarifa hii, Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu Umma kwamba Majukwaa na Programu Tumizi "Applications" zifuatazo hazina kibali na haziruhusiwi kuendelea na shughuli za utoaji mikopo kidijitali;

Previous Post Next Post