Na Lilian Ekonga, Dar es salaam
Katika Kipindi cha Miezi Mitatu kuanzi Julai hadi Septemba 2024, Mamlaka ya Mapata Tanzania TRA imekusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 7.79, sawa na ufanisi wa asilimia 104.9 ambapo lengo lilikuwa kukusanya Shilingi Trilioni 7.42, na kuvuka lengo la kila mwezi kwa miezi yote mitatu.
Alikalika kwa kipindi cha mwezi Septemba TRA imefanikiwa kukusanya kiasi cha Shilingi Trilioni 3.02, sawa na ufanisi wa asilimia 105 ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 2.88.
Ameyasema hayo Leo Octobar 1 Jijin Dar es salaam, Kamshina Mkuu wa TRA, Yusuph Juma Mwenda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari,ambapo amesema ukuaji huo katika makusanyo umechangiwa na Kuendelea kutekeleza kwa vitendo maagizo na maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
"kuhamasisha ulipaji kodi wa hiari nchini kwa Kushirikiana na Walipakodi, kuwasikiliza na kutatua changamoto za walipakodi wote nchini, pamoja na kukua kwa uchumi wa nchi pamoja na ongezeko la wawekezaji kutokana na uwepo na usimamizi wa será nzuri za uwekezaji za serikali ya awamu ya sita"amesema
Ameongeza kuwa "Kuendelea kuboresha mahusiano na wafanyabiashara kwa kutenga siku ya Alhamisi ya kila wiki kuwa ni siku maalum ya ‘Kusikiliza Walipakodi’ kupitia ofisi zote za TRA nchini"
Aidha amesema Ufanisi wa makusanyo uliofikiwa na TRA kwa miezi ya Julai – Septemba ni kiashiria chanya katika kuhakikisha kuwa lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 la Shilingi Trilioni 30.04 linafikiwa.
" Katika kufanikisha hili TRA Itatekeleza Ku maagizo yote ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu usimamizi wa kodi nchini na uhamasishaji wa ulipaji kodi kwa hiari" amesema
Pia amesema wataendelea kusimamia na kuimarisha misingi ya mfumo mzuri wa kodi, ikiwemo Haki na Usawa katika utozaji kodi (no favouritism or victimization) ili kuweka mazingira ya biashara yaliyo sawa.
Kadhalika Kamshina Mkuu amewashukuru walipa kodi Watanzania pamoja na Walioajiriwa na ndio waliowezesha kukusanya hizo Trilioni 3 ndani ya mwezi wa tisa na kutuwezesha kukusanya Trilion 7.79 ndani ya miezi mitatu ambapo ni ukuaji wa asilimia 15 pamoja na wafanyabishara wadogo ,wakati na wakubwa kwa kuitikia kulipa kodi.