NHC YAZIDI KUPATA FAIDA KWA MWAKA 2024 / 25


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba  la taifa (NHC), Hamad Abdalla amesema kuwa hadi kifikia juni, 2024 mtaji wa shirika hilo ulikuwa sh trilioni 5.6 ikilinganishwa na mwaka uliopita shiling trilion 5.04

Aidha amesema thamani za mali na shirika zinaendelea kukua mwaka hadi mwaka kutokana na usimamizi na maendeleo mazuri wanayopata kutola serikalini na chama tawala

Mkurugenzi Mkuu ameyasema hayo leo octaba 13, 2024 katika wasilisho lake kuhusu majukumu na mafanikio ya shirika la nyumba katika mkutano wa viongozi wa jimbo jijini Dar es salaam.

"Kwa mafanikio haya inamaana chomba kinachosimamia serikali kinafanya kazi yake.Na ndani ya shirika la nyumba tunafanya vizuri"

Amesema jitihada za shirika katika  kuwekeza na kutekeleza miradi mbalimbali imekuwa ikiwezesha serikali kupata gawio kubwa

Katika hatua nyingine amesema kuwa ndani ya miaka mitano kuanzia 201/19-2023/24 mapata ya shirika yamekuwa kutoka bilioni 125 kwa mwaka hadi shilingi bilioni 184 kwa mwaka sawa na ongezekola asilimia 47 kwa mwaka.

Aidha amewaelekeza viongozi hao kuwa, majukumu ya shirika hilo yanatekelezwa kwa kuzingatia mpango mkakati wa miaka 10 wa NHC ambao ulianza mwaka 2015/16-2024/2025

Katika hatua nyingine Mkurugenzi mkuu amesema ilalani miongoni mwa maeneo nchini ambapo shirika hilo linatekeleza miradi mingi ya kihistoria kupitia sera ya ubia na tayari matokea yameshaanza kuonekana.

"Ilala inakwenda kuwa kama Dubai, Tunajenga miradi inayozingatia kasi ya viwango vya kimataifa"
Previous Post Next Post