ZAIDI YA MALALAMIKO 1500 YAMESHUGHULIKIWA KISHERIA KUPITIA KITUO CHA HUDUMA KWA MTEJA





Na Lilian Ekonga....

Wizara ya katiba na Sheria kupitia kituo cha Huduma kwa Mteja kuanzia mwaka 2024 hadi july 2025 kimepokea malalamiko 1508 ambapo asilimia 66 yameshafanyiwa kazi na kuhitimishwa huku asilimia 34 yakiwa katika hatua yakufanyiwa kazi na kuhitimishwa


Akizungumza katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya Biashara (sabasaba) Wakili wa Serikali na Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja kutoka Wizara ya katiba na Sheria, Judica Nkya amesema kituo cha hicho kinahudumiwa na wanasheria wabobezi ambao wanahudumia wateja kwa njia simu, massage, email na mitandao ya kijamii.

"Kituo kimeunganishwa na Taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kwajili ya kuhudumia wateja katika shida mbalimbali zinazo wasilishwa Wizarani" amesema Nkya

Ameongeza kuwa Wizara pia inapokea malalamiko wa njia ya Barua ambazo zinaletwa kwa njia ya Posta na walalamikaji wengine wanapekeleka moja kwa moja wizarani nayo yanashughulikiwa kupitia kituo cha Huduma kwa Mteja

Amesema Katika Malalamiko 1508 Maeneo yaongoza katika kulalamikiwa zaidi ni Eneo Ardhi pamoja na Miradhi ambapo shida imekuwa katika uelewa wa sheria na taratibu za kufungu kesi na kusimamia Miradhi.

"Wananchi Wengi katika Mambo ya Miradhi bado hawajajua tararibu za kufungua kesi, kusimamia miradhi na watupigia simu tunawaelezea taratinu wanazotakiwa kuzifuata na wengine tunawaelimisha kuwapa taratibu za sheria za kusimamia Miradhi" amesema Nkya

Aidha amesema mikoa inayoongoza kwa kuripoti malaamiko katika kituo huduma kwa mteja ni Mkoa wa Dar es salaam ukifuatiwa na Njombe.

"Unaweza kupitia simu kupitia kituo cha Huduma kwa Mteja kupitia Namba 0262160360 na kwanjia ya whatsp utatupata kwa namba 0739101910 na email malalamiko@sheria.go.tz"
Previous Post Next Post