TATU MZUKA YAZINDUA KAMPENI YA 'BOSS KARUDI' MILIONI 300 KUTOKA MSIMU HUU


Kampuni ya  Tatu Mzuka imezindua  kampeni  mpya ya 'BOSS KARUDI ' ambayo kwa msimu huu wanaenda kutoa Milioni 300 kwa mara moja kwa Mtanzania atakaye bahatika kushinda.

Akizungumza na waandishi wa leo Septemba 12, Mkuu wa bidhaa kutoa Tatu Mzuka, Jackline kaboko amesema kupitia Droo za zao kila dakika 5 mtanzania anaweza kushinda kuanzia  laki mbili mpaka milioni 6.

 Kutakuwa na Jackpot mbili kubwa, jumatano kutakuwa na jackpot milioni 20 ambayo itaenda kwa mtanzania ambaye atabahatika pia kuna bidhaa tutakazo toa kama bodaboda, bajaji, smaprtphone, latpot na itakuwa ikionyesha jumatano saa 3 usiku pale Clouse TV." Amesema

Jackline ameongeza kuwa kutakuwa na jackpot ya jumamos ambayo watato milioni 50 kwenda kwa watanzania ambao watabahatika na itaonyesha kupitia Television ITV.

Aidha amesea lengo la kutoa hizo pesa ni kuhakikisha wanasaidia kukuza  maisha ya kila mtanzania kwenye  nyanja za uchumi.

"Kuhusu usalama wa Pesa zenu watanzania, tuhakikisha kwamba pesa zako utazipata kwa utaratibu mzuri kabisa na Tatu mzuka ukishanda  hauta tuma kiasi chochote kile ili uweza kupata yako, sisi ndo tutakupigia na kukupa utaratibu.

Kwa upande wake balozi wa Tatu mzuka Gea Habibu amesema Ule mzuka Mzuka wa Daily unarudi tena na msimu huu mshindi atajinyakulia kitita cha milion 1 kila siku kasoro simu ya jumatano na jumamosi ambazo ndizo za jackpot Kubwa.
Previous Post Next Post