ONYESHO LA NANE LA 'SITE' KUFANYIKA OKTOBA 11 HADI 12 MWAKA HUU


Na Mwandishi wetu

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) katika kutangaza Vivutio vya Utalii na fursa mbalimbali za Uwekezaji zilizopo Nchini imeandaa Onesho la nane la Site kwa mwaka 2024 litakalofanyika kuanzia 0ktoba 11 hadi 13 mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Akizungumza  leo Septemba,12 2024 Jijini Dar es na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu  wa TTB, Ephraim Mafuru alisema Onesho hilo litahudhuriwa na waoneshaji wa bidhaa na huduma za Utalii zaidi ya 120 sambamba na wanunuzi wa bidhaa na huduma za Utalii takribuni 120 kutoka Nchi ambazo  ni kimkakati ya utalii wetu ikiwemo  nchi za Asia, Ulaya  na Amerika.

Alisema onesho hilo litshusisha utangazaji  wa bidhaa mbalimbali za utalii, jukwaa la uwekezaji, semina kuhusu masuala ya utalii na masoko na mikutano  ya wafanyabiashara za utalii.

"Onesho la Site linakwenda sambamba  na utekelezaji  wa Sera ya Taifa  ya Utalii ya mwaka 1999 pamoja na mkakati  wa kutangaza utalii kimataifa  2020 -2025 ambayo imetilia mkazo kuitangaza Tanzania  kam kivutio bora cha utalii duniani,"'alisema.

Alieleza kuwa Onesho hilo linafuatiwa na ziara  za mafunzo "FAM trips" ambayo yanalenga  kuwajengea  uelewa  wanunuzi wa hidhaa na huduma  za utalii kuhusu vivutio vyetu vya utalii ili waweze  kuvitangaza katika nchi zao na dunia kwa ujumla. 

Alitoa rai kwa wadau  wa utaliii Waliopo ndani na nje ya nchi hususani  Wakala  wa biashara  za utalii,watoa huduma za malazi, Wakala wa safari  na zingenezo  kushiriki  na kuchangamkia fursa za kiuchumi  na kijamii zitokanazo na Onesho la Site 2024.
Previous Post Next Post