AIRTEL MONEY YAWAZAWADIA WATEJE WAKE BONASI YA 20,000 KUPITIA KAMPENI MPYA YA JIBOOST


Na Lilian Ekonga

Kampuni ya Mtandao wa  simu Airtel Tanzania leo imezindua promosheni mpya ya ‘JiBoost na Airtel Money’ ambayo i nawapa nafasi watumiaji wa Airtel Money kujipatia shilingi 20,000 taslim ya supa bonasi kupitia miamala ya kila siku watakayofanya. 

Aidha Mpango huo ni sehemu ya maono ya kampuni ya Airtel katika kupanua huduma ya Airtel Money na kujenga huduma za kifedha jumuishi na wezeshi kwa wateja wake. 

kizungumza na Wandishi wa Habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba amesema  Promosheni hii imetengenezwa kuwasaidia  wateja wao  kila wanapotumia huduma za Airtel Money katika Maisha yao ya kila siku kama manunuzi ya vifurushi

 "Wateja wetu watakuwa wakinufaika zaidi na kila muamala watakaofanya. Tunajivunia kuwa vinara wa kutoa huduma suluhishi kupitia Airtel Money kwa wateja wetu.” amesema Rugamba

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano, Airtel  Jackson Mbando  amesema Kampeni ya JiBoost ya Airtel Money inamruhusu Mteja kuweza kupata supa bonasi ya shilingi 20,000 kupitia muamala unaotumwa Kwenda kwa mtu mwingine, kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi, malipo ya LUKU, malipo ya serikali na kununua vifurushi vya king’amuzi. 

" Kila mteja atakapokamilisha muamala unaostahili, atapokea ujumbe wa maandishi ukithibitisha kuwa amepata bonasi. Kila mteja atakapokuwa akifanya malipo atakuwa anapata gawio la bonasi hadi itakapofikia thamani ya shilingi 20,000. Kila bonasi atakayopata mteja itaonekana kwenye akaunti yake ya Airtel Money ikiambatana na ujumbe wa SMS utakaoonyesha mwenendo wa bonasi hizo." amesema Mbando.

Nae Kwa upande wake, Joti ambae alivaa uhusika wa Mr Money, amesema "Kama Mr Money, naweza kukuambia kuwa kampeni hii ni mahususi kwa ajili ya kurudisha pesa kwenye mfuko wako. Kila utakapofanya malipo ya TV, umeme na kununua muda wa maongezi, unakuwa unajipa nafasi kubwa zaidi ya kupata bonasi. JiBoost ipo hapa kwa ajili ya kufanya miamala yako ya kila siku iwe ya furaha na yenye zawadi.”
Previous Post Next Post