ZAIDI YA VISIMA ELFU MOJA VIMECHIMBWA KWENYE MWAKA WA FEDHA 2023/24


Na Mwandishi Wetu

TUME ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na uchimbaji wa visima 1000 kwa nchi nzima katika mwaka huu wa fedha 2024/ 2025.

Mhandisi kutoka Tume hiyo, Naomi Mcharo amesema hayo katika maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi yajulikanayo kama nane nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.

Amesema uchimbaji huo utamwezesha mkulima wa Tanzania kulima kilimo cha umwagiliaji, kwa kulima mara mbili mpaka tatu kwa mwaka badala ya kutegemea mvua ili ajitosheleze kwa chakula.

Kutokana na jitihada hizo za serikali, Naomi amewaalika wananchi katika banda la tume hiyo, kwa ajili ya kupata maelezo ya kina kuhusu maeneo ya  uchimbaji visima, vikundi gani vinahusika katika kuchimba visima na kuweka miundombinu ya umwagiliaji.

"Kwa hiyo tunawakaribisha sana katika banda letu ili mjionee teknolojia mbalimbali za umwagiliaji. Muweze kujionea miradi ambayo tunaendelea nayo katika mwaka huu wa fedha," amesema.

Amesema wananchi katika banda la tume hiyo watajionea miradi inayotekelezwa nchi nzima ikiwemo ya uchimbaji wa visima, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya umwagiliaji .

"Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, imejipanga na inaendelea na utekelezaji wa azma yavRais Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kujitosheleza  kwa chakula, kuilisha Afrika na kuilisha dunia," amesema.
Previous Post Next Post