WIKI YA AZAKI KUWAKUTANISHA WATU ZAIDI YA 500 ARUSHA


Na Lilian Ekonga, Dar

WIKI ya Asasi za Kiraia inatarajiwa kufanyika kuanzia Septemba 9 hadi 13 jijini Arusha.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 23, 2024 na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la CBM  International Nesia Mahenge akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam.

Mahenge amesema kuwa kwa mwaka huu wiki hii ya AZAKI itawakutanisha watu zaisi ya 500 ambapo kauli mbiu ni "Voice, Vision and Value" (Sauti, Dira na Thamani).

"Wiki hii tunakutana kwa ajili ya kuzungumza kuhusu wiki ya AZAKI, tunaangalia changamoto na tunaangalia kama AZAKI na Serikali namna gani tushirikiane kwa ajili ya ma ndeleo," amesema Mahenge na kuongeza,

"Wiki ya AZAKI itafanyika Septemba 9 hadi 13, 2024 na itafanyika Arusha Mount Meru, itakuwa na mambo mengi na tunaangalia thimu ya Sauti, Dira na Thamani na kutakuwa na watu zaidi ya 500,".

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji w Foundation For Civil Society Justice Rutenge amesema sababu ya kuwa na thimu hiyo kwa mwaka huu ni Kutokana na kwamba tupo katika kipindi muhimu cha Demokrasia.

Kwamba mwaka huu baadaye kuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa na mwakani Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani huku pia mwakani Tanzania ikitarajia kizindua Dira ya Taifa ya mwaka 2025/2050.

Kuhusu Dira ya Taifa Rutenge amebainisha kuwa pamoja na tofauti tulizo nazo kama Watanzania mwisho wa siku Dira ni maoni ya Watanzania.

Kwamba kwa upande wa Thamani amesema ni muhimu kuwa na Utekelezaji wa Dira ya Taifa ili kifikia Maendeleo ya Taifa ambapo amebainisha kuwa katika Wiki ya AZAKI Thamani itapatikana kwa kushirikiana na nyanja mbalimbali.

"Kutakuwa na ushuriki wa Serikali, Sekta binafsi, Sekta ya Umma, mashirika mbalimbali ya ndani na kimataifa na wananchi," amesema Rutenge.

Naye Mkurugenzi wa Ubongo, Mwasi Wilmore amesema wamefurahi kuwa sehemu ya washiriki wa wiki hii na kwamba ni furaha kuwaleta watu pamoja kutoa maona yao namna ya kuijenga Tanzania.
Previous Post Next Post