TPDC YAJIPANGA KUANZISHA VITUO VYA GESI PWANI, MOROGORO, DODOMA


Na Humphrey Msechu

MKUU wa Kitengo cha uhusiano na Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Marie Msellemu amesema , katika mwaka huu wa fedha ,Shirika hilo  limepanga kuanzisha vituo vya gesi asilia mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma.

Musellemu ameyasema hayo wakati akizungumza na waandiahi wa habari kwenye maoneaho ya wakukima na wafugaji yanayoendelea katika viwanja vya 88 jijini Dodoma.

Amesema hatua hiyo itasaidia mtu kusafiri 
kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma kwa kutumia gesi asilia badala ya mafuta kwasababu ni rafiki kwa mazingira huku akisema hatua hiyo itasaidia watu wengi zaidi kuendelea kubadilisha mifumo ya magari yao kutoka kwenye matumizi ya mafuta  kwenda kwenye gesi.

"Vituo hivyo vitasaidia mtu kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Dodoma kwa usafiri unaotumia gesi asilia. Usafiri huu ni mzuri na salama kwasababu hautumii gharama kubwa na ni rafiki kwa mazingira,"alisema

Na Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe Sophia Mwakagenda aliipongeza serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais DKT.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi.

Amesema serikali imeendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kujenga vituo vya kujazia gesi asilia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo Kwa wananchi.

"Serikali ya Awamu ya Sita inastahili pongezi  kwa kuendelea kuweka Nguvu kubwa katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi na Sasa serikali inaendelea kujenga vituo vya kujazia gesi hiyo ili kuwahakikisha wale wote waliobadilisha mfumo kutoka katika matumizi ya mafuta kuwa huduma hiyo  ipo,"amesema Msellemu

Previous Post Next Post