TIGO WAENDELEA KUTOA ELIMU YA TIGO PESA KWA WANAWAKE WAJASIRIAMALI



Na Sharon Lucumay, Dar es salaam

Kampuni ya simu ya tigo wamefanya mkutano na wafanyabiashara wanawake kutoka kariakoo kwa dhumuni la kuwaelezea huduma za tigo na kusikiliza changamoto mbalimbali wafanya biashara hao wanazozipitia.

Hayo wamesemwa leo jijini Dar Es Salaam na Afisa mkuu wa Tigo Pesa Anjelika Pesha ameeleza mkutano huu umetoa elimu na manufaa ya huduma mbalimbali za tigo kwa wafanyabiashara wanawake wa kariakoo ( kariakoo business women ) ikiwa ni pamoja na huduma ya lipa kwa simu ambayo inasaidia kutunza kumbukumbu na kuwa na miamala ya kidigitali. 

Aliendelea kwakusema kuwa mkutano huu umesaidia kuona ni changamoto gani wafanyabiashara wanawake wa kariakoo wanazozipitia ambazo watazifanyia kazi kwa kupanga mpango mkakati mfupi na mrefu ilikualsaidia kuwawezesha wanawake waweze kufanya biashara kiurahisi na salama kupitia tigo pesa ilikufikia uchumi wa kidigitali. 

 " Huu ni mwanzo tuu kwan tigo inampango wa kwenda mkoa hadii mkoa kutoa elimu na huduma za tigo pesa kwa wafanyabiashara wotee makubwa na wadogoo hasahaswa wanawake ikiwa ni katika juhudi za kuunga mkono serikali kuhakikisha wanafikia makundi ambayo yanahitaji masada wakifedha kujikwamua kiuchumi haswahaswa wanawake" alisema  Anjelika Pesha, Afisa mkuu wa tigo pesa.

Francisca Joseph Mfanyabiashara na mwenyekiti wa Kariakoo business women ameeleza kuwa kupitia kikaoo hichii kimewafungua akilii zao katika swala zima la uwrkaji wa akiba na utunzaji wa kumbukumbu za mauzoo kupitia huduma ya lipa namba.

 Ameeleza elimu hii waliyoipata wamejifunza mengi na wataifanyia kazi na kuendeleza kwa wafanyabiashara wengine kwani tigo imeweza kuheshimisha wanawake wafanyabiashara wa kariakoo. 

Kampuni ya mawasiliano ya tigo imekutana na Zaidi ya wanawake wafanyabiashara 35  kutoka eneo la biashara kariakoo lakini pia huo ni mwanzo tu,matarajio yao ni kukutana na wafanyabiashara wote nchini ili kusaidia kuleta ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania wote.

Previous Post Next Post