FCS WAIOMBA SERIKALI KUWEZESHA MAKUNDI MAALUMU KUFIKIA MIUNDOMBINU YA KIDIGITALI


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam.

Meneje Programu wa  Asasi za Kiraia (FCS)  Nasim Losai ameiomba serikali iangazie katika kuwawezesha  makundi maalumu katika   kuweza kufikia miundombinu ya kidigitali ili waweze kufanya maamuzi sahii na kushiriki katika michakato ya maendeleo na kuimarisha uchumi wao.

Hayo ameyasema leo Agust 12 katika Mkutano wa kitaifa wa watu wenye  ulemavu, madiwani na wadau uliofanyika jiji la Dar es salaam.

Ambapo amesema mkutano huo umejikita katika kuangazia ushiriki wa watu wenye ulemavu  katika maendeleo, uchumi na kijamii huku ukiangazia matumizi ya takwimu za sensa katika kuboresha  mapango wa halmashauri za wilaya  na ngazi za kata.

"Serikali imekuwa sikivu na sana na sisi foundation tunazaidi ya miak 20 tumekuwa tukisaidia serikali hasa katika shughuli za kutetea watu wenye ulemavu na michakato ya kiserikali hasa kwenye majengo mengi sana mioundombinu imebadilika  na kazi kubwa imefanywa na fsc pamoja na makundi haya" amsema Losai

Kwa upande wake Peter charlse Mshauri wa kiutalamu wa maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania  amesema mkutano huo umejuisha watu  mwenye ulemavu  600 kutoka ndani ya jiji la Dar es salaam wakiwepo madiwani 60 wa viti maalimu na wakuteuliwa.

Ameongeza kuwa  Malengo ya mkutano huo ni kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu katika maswala ya sensa, uchumi na fursa na utakwenda kuangazia zaidi maswala ya uchumi na kuona  fursa zipi  walemavu wameweza kushirikishwa na wao wameweza 

"Ushirikishwaji wa watu wenye ulemavu bado ni mdogo ndomana wakamamuu kuwalika madiwani katika mkutano huo ili  kuangalia changamoto ipi wapi na kuwajengea uwezo madiwani ili kuweza kuwashirikisha madiwani katika mipango yao ya maendeleo kupitia mabaraza yao ndani ya halmashauri" amesema

 
Nae Hamadi Abdallah komboza, mwenyekiti wa Taifa wa chama cha walemavu Tanzani amesema  changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu ni maswala mazima ya ajira huku akimuomba kamshina wa kazi  na vyama venye ulemavu kufanya ukaguzi kwenye mashirika na taasisi ambazi zinapasqa kuajiri watu wenye ulemavu lakini bado hazija kidhi ili kuweza lueta msukumo zipelekwa mahakamani ikibidi ili watu wenye ulemavu waweza kuajiriwa.

Jonas Lubalo, katibu  mkuu shirikisho la vyama vyenye ulemavu Tanzania amesema Wanaishuru Taasis ya Ikupa Trust Fund kwa kuendelea  kuchangia kutoa huduma za kwa watu  wenye ulemavu kwa namna anavyotoa misaada  kwenye maeneo mbalimbali ya watu wenye ulemavu.
Previous Post Next Post