KAMPUNI YA LUMINOUS POWER TECHNOLOGIES YAINGIA MAKUBALIANO NA KAMPUNI SWAMINATH TRADING


Na lilian Ekonga

Kutokana na mazingira mazuri ya kibiashara ambayo yamewekwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imepelekea Kampuni ya Luminous Power Technologies kuingia makubaliano na Kampuni ya Swaminath Trading ili waweze kuuza bidhaa zenye ubora wa kimataifa zinazotumia umeme wa jua.

Vifaa hivyo ni pamoja na Inverter maarufu za Optimus, Betri za SMF, inverter za Solar na Battery za Tubular

Akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais, Biashara ya Kimataifa, Luminous Power Technologies Revanand Andhale alisema kutokana na uwepo wa ongezeko la mahitaji ya umeme nchini, wana imani kuwa kufaa hivyo vitaenda kuondoa changamoto hiyo kwa asilimia kubwa.

“Tunafuraha kuanza safari hii na Swaminath Group kwa kushirikiana na Tandhan Group, na kujikita kwa dhati kutoa vifaa vya kuaminika na vyenye ubunifu wa hali ya juu na kuwaletea watanzania suluhisho la kudumu la upatikanaji wa nishati kwa watanzania”

“Kuna ongezeko la mahitaji ya umeme nchini, na tuna imani kuwa vifaa vyetu vitapokelewa vyema nchini, bidhaa zetu zinaaminiwa na mamilioni ya watumiaji duniani kote na tunataka watanzania pia wanufaike kuoitia utumiaji wa vifaa vyetu”

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Swaminath Group, Mayur Dilesh Solaki alisema kupitia ushirikiano huo, wamelenga kuendelea kuwapa wateja wao suluhisho la muda mrefu kwa vifaa vya kisasa vyenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu ikilinganishwa na bidhaa shindani.

“Ushirikiano wetu wa Luminous unaturuhusu kuleta vifaa vya umeme mbadala vyenye viwango vilivyothibitshwa kuwa na ubora was kimataifa, ushirikiano huu unaonyesha kujitolea kwetu katika kuendeleza teknolojia na kukuza nishati endelevu hapa nchini Tanzania, tumelenga kuendelea kuwapa wateja wetu suluhisho la muda mrefu kwa vifaa vya kisasa vyenye ubora wa hali ya juu na kwa bei nafuu ikilinganishwa na bidhaa shindani” Amesema

Emma Laswai kutoka Jumuhiya ya wadau wa Nishati jadidifu Tanzania (TAREA) alisema wakazi wengi waliopo Jijini Dar es Salaam huenda wakawa wanatumia umeme wa Tanesco lakini kuna jamii ambazo bado hazijafikiwa na umeme huu hivyo uwepo wa wadau hao kunapelekea kuhakikisha yale maeneo ambayo hayajafikiwa na umeme waweze kupata Nishati ya umeme kwaajili ya matumizi yao binafsi lakini pia matumizi yao ya biashara.

“Pia kuna baadhi ya matumizi, kwenye sekta ya afya, vyuoni na viwanda hivyo tunaamini teknolojia hizi ni rafiki wa mazingira na ndiyo maana zinaitwa teknolojia ya kijani ambapo zinasaidia kulinda mazingira na kupunguza viwango vya hewa chafu nchini”

Aidha alisema kwa tafiti zilizofanywa na serikali kupitia ofisi ya mtakwimu au wakala wa Nishati vijijini mwaka 2023 ilionesha kwamba siyo kila mmoja amefikiwa na umeme mbalimbali ambapo asilimia 40-45 wamefikiwa na umeme ambapo Tanzania ina watu Milioni 60.

“Wale waliobaki hatuwezi kusema tuansubiri solution moja kwa wote haitafika kwa wakati mmoja, inawezekana wengine wakafikiwa mwaka huu, wengine baada ya miaka miwili mpaka kumi, wale ambao wanaweza tunahamasisha waanze kujikwamua kwa kutumia teknolojia hizi ambazo ni rafiki wa mazingira kwasababu zinapatikana ukijipanga zinaweza kununulika kuanzia ngazi ya Kaya mpaka taasisi mbalimbali zinazopatikana katika maeneo yao”

“Bado soko ni kubwa, bado tunahitaji wadau zaidi kufika na wale wahitaji wa hizi Nishati na wao wanasubiria kwa hamu kwasababu ukifikiwa na umeme ni sawa na

Umefikiwa na maendeleo” Amesema

Previous Post Next Post