JKT yaeleza siri ushindi wa jumla maonesho nane nane



Na Humphrey Msechu, Dodoma

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limepata ushindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya wakulima ,wafugaji na uvuvi (88)  yaliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya maadhimisho ya siku hiyo,Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab amesema,siri ya ushindi huo ni bidii waliyoionesha katika maandalizi ya maonesho hayo.
Amesema ,JKT limeyapa umuhimu maonesho hayo kwa namna ya pekee na kwamba wamekuwa wakifanya shughuli za masuala ya kilimo na ufugaji na uvuvi katika viwanja vya Nane Nane hata baada ya maonesho kumalizika.

"Mahali hapa sisi ni pa kudumu, na siyo tupo wakati wa maonesho tu, na ushindi wowote ni bidii,hata mwanafunzi anapokuwa shuleni ,ili afanye vizuri anatakiwa kufanya bidii na ndiyo maana tumechukua ushindi huu na hata mwaka jana hapa Dodoma tulishinda nafasi ya kwanza,

Meja Jenerali Mabele amesema ,katika maonesho hayo JKT imeshiriki sekta zote zikiwemo za kilimo,ufugaji na uvuvi  ambapo vijana wa JKT wameshiriki katika shughuli hizo huku akisema ujuzi wanaoupata pia utawadaidia baada ya kumaliza mkataba wao na kurejea uraiani.
"Katika kilimo,tunaonesha kilimo bora  bora ,katika mazao ya bustani wanalima kitaalam ,lakini pia katika eneo la mifugo nako  tunao ng'ombe wetu na mifugo mingine ambayo pia tunafuga kitaalam,

"Ukija katika eneo la uvuvi na ufugaji hali kadhalika tunafanya vizuri,tunazo teknolojia ya ufugaji samaki wa matenki ambao sisi JKT ndiyo tulianzisha Teknolojia hii na kuipeleka katika maonesho mbalimbali ambayo sasa hivi inafanywa na wengi."amesema Meja Jenerali Mabele

Previous Post Next Post