WILAYA ZAIDI YA 98 NCHINI ZIMEPATA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO


Na Humphrey Msechu, Dar

Shirika la mawasiliano la TTCL katika maonesho haya ya kimataifa ya biashara saba saba imepata ata fursa mbalimbali ikiwemo kuonesha bidhaa zake kile  kinachokifanyika, pia imeweza kukutana ana kwa ana na wateja wake na  kutoa elimu,  huduma na uelewa kuhusu kazi na wajibu wa shirika hilo.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa T- PESA Lulu Mkudde Uku akiwaeleza wananchi juu ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na TTCL ambayo ni mkongo wa Taifa wa mawasiliano na kutoa mafunzo mbalimbali na kuweza kutoa mafunzo kuhusu hudma za mkongo wa Taifa lakini pia wana kituo mahiri cha kutunza kumbukumbu, pia na  huduma  za T Pesa 

Lulu Mkudde Amesema kuwahakikishia wafanya biashara na wawekezaji kuwa huduma hizo ni wezeshi katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema Katika kuunga mkono kauli mbiu ya maonesho ya mwaka huu wao wameona  watumie fursa hii kufungua milango kwa wawekezaji na wafanyabiashara kufanya kazi zao kidigitali ambapo huduma hizo hapa Tanzania zilikuwa zikielezea  ni kwa namna kazi zinaweza kufanyika kidigitali na hivyo kuleta ufaanisi na matokeo chanya.

Shirika limekuja na huduma ya mtandao (WiFI  T Cafe ) ambayo imelenga  kuwaondolea adha wafanyabiashara waandishi  wa habari na wataalam wa masuala ya ushauri na yeyote anayetaka kufanya kazi nje ya ofisi yake ,ni fursa kwake kuja kutumia huduma za T-CAFE kutekeleza majukumu yake", amesema Lulu Mkudde 

Shirika linaanzisha huduma hii ili kuwawezesha walengwa wote kufanya shughuli zao kwa gharama nafuu

Amesema Katika kipindi chote cha maoneaho haya huduma hii Imefanya kazi  kwa viwango vya hali ya juu sana.

Ameongeza kuwa kwaasa Huduma ya fiberinaweza kukufikia nyumbani kwako kwa gharama nafuu

Pia wanaendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya Fiber na wamepokea maombi mapya mengi wanaohitaji huduma ambayo imekuja kuleta mapinduzi ya kuisha haraka kwa vifufushi vya kawaida ambapo sasa shirika limeleta huduma hii ambayo inamwezesha mteja kutumia internent ambayo haina ukomo.

Amesema Hapo nyuma walikuwa wakisikia kwamba vifufushi vya internet vinaisha kwa haraka kwa hiyo huduma hii yenyewe haina ukomo

Ameongeza  wananchi ambao bado hawajaomba nafasi hiyo kutumia tovuti  www.ttcl.co.tz kisha taarifa zao zitachukuliwa na kuanza mchakato wa kuwafungia huduma hiyo 

Tunaposema tunafungua milango kidigitali tunamaanisha kuweka mazingira wezeshi hapa nchini ya kimtandao ", amesema Lulu Mkudde.

Mpaka sasa shirika limefanya mambo mengi ikiwemo huduma ya T PESA ambapo wamekuja na huduma ya akaunti portal ambayo inamwezesha mteja kufungua akaunti ya T PESA  bila kuwa na hitaji la sim card

Kwa hiyo anapopakua  app ya T PESA kupitia play store ana uwezo wa kufungua akaunti yake hata akiwa nyumbani na kufanya huduma zote za kifedha kwa njia ya kupitia app yake ya T PESA 

Amesema Hadi sasa mkongo wa Taifa umesambazwa katika mikoa yote nchini huku zaidi ya wilaya 98 zikiwa zimeshafikishiwa mkongo wa mawasiliano ambapo juhudi hizo zote zinalenga katika upatikanaji wa huduma ya elimu ,afya na maendeleo kwa ujumla yanatekelezeka kidigitali katika maeneo yote nchini.

Amewahakikishia wananchi kwamba TTCL itahakikisha huduma za mawasiliano zinakuwa nzuri ili kuwapa fursa wananchi kupata huduma mbalimbali  lakini nao kujiingizia kipato kupitia mtandao bora wa TTCL kwa gharama nafuu.
Previous Post Next Post