MFUMO WA eGA KURAHISISHA UTATUZI WA KERO KWA WANANCHI


Na Humphrey Msechu, Dar

Wananchi wametakiwa kutumia mfumo wa e- mrejesho katika kuwasilisha changamoto zao kwa Serikali na kutoa hoja zao ili ziweze kufanyiwa kazi.

Rai hiyo imetolewa na Mamlaka ya Serikali e- mrejesho katika mtandao wake wa (eGA) kwa lengo la kushughulikia changamoto za wananchi kwa haraka zaidi.

 Akizungumza na waandishi wa habari katika banda la eGA kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba)  jijini Dar Dalaam, Meneja  Mawasiliano wa  eGA Subira Kaswaga amesema suala la kujenga mifumo kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi katika utumishi wa umma ni jukumu la eGA  huku akisema katika jukumu hilo imejenga mfumo wa  mrejesho ambao ni daraja la mawasiliano batons ya wananchi na Serikali

Amesema kupitia mfumo huo, wananchi wanaweza kuelezea kero na changamoto yoyote ,maoni ,kuuliza swali lolote au hata kuongea na Serikali na yote kwa pamoja yatafanyiwa kazi na Serikali.

"Mfumo unapatikana kwa njia ya simu ya mkononi kwa kubonyeza *152*00# halafu namba 9 na kuendelea kufuata maelekezo na taasisi zote za Umma zimeunganishwa katika mfumo huu wa e-mrejesho,kwa hiyo mwananchi akiwa na kero mbalimbali anaweza kuwasiliana na Serikali ikazifanyia kazi." amesema Kaswaga

Kwa mujibu wa Kaswaga huduma hiyo inapatikana kwa  kupakua app ya e-mrejesho au kwa kutumia tovuti ya www.emrejesho.co.go.tz,

Aidha amesema kutokana na utendaji wake, mfumo  huo umetambuliwa kimataifa kwamba ni jukwaa huru ambalo linawasaidia wananchi kuwasiliana na serikali na kupitia mfumo huo eva inaweza kushindwa tuzo katika Umoja wa Mataifa ya ubunifu wa huduma za umma mwaka huu 2024 ambazo zilitolewa nchini Korea.

"Kwa hiyo nitoe rai kwa wananchi kuutumia lakini pia taasisi za umma zihamasishe wadau wake kwa maana ya wananchi wanaowapa zile huduma watumie zaidi mfumo wa e mrejesho kuwasilisha maoni yao."amesisitiza Kaswaga 

Vile vilenameaema taasisi hiyo pia imejenga mfumo wa kubadilishana taarifa serikalini kwa maana ya mifumo kusoma kwa lengo la kurahisisha na kuboresha uwajibikaji seeikalini.

"Kama tunavyofahamu kwamba mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza taasisi za umma kubadilishana taarifa kidigiti , kwa hiyo sisi kama mamlaka tumetengeneza mfumo huo  na tayari tumeshaunganisha mifumo mbalimbali na sasa wanachokifanya ni kuzihamasisha taasisi za umma ziweze kujiunga na mfumo huo ili ziweze kubadilishana taarifa."

Kwa mujibu wa Kaswaga  mpaka sasa  taasisi ambazo zimeunganishwa na mfumo huu ni taasisi 141 na mifumo 148 imeshaunganishwa na katika hiyo mifumo 109 inasomana na kubadilishana taarifa.

"Kwa hiyo tunafanya jitihada mbalimbali ikiwa ni pamoja na ofisi za umma kuziunganisha kwenye mfumo huo  na  July 22-29 tunatarajia kuwa na kikao na taasisi za umma taktiban 70 kwa lengo la kuwapa  elimu kuhusiana na mfumo huo lakini pia kuunganisha ili hizo taasisi zijiunge na mfumo huo wa kubadilishana taarifa."amesisitiza

Previous Post Next Post