FCC YAKUTANISHA WADAU KUJADILI NAMNA YA KUMLINDA MLAJI(AKILI MNEMBA)


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam.

Tume ya ushindani (Fcc) imeomba serikali  kupitia  mamlaka zake kuweka utaratibu wa kiudhibiti utakao wataka watoa  huduma kupitia mfumo  ya teknolojia kuweka bayana  changamoto zinazoweza kujitokeza kwa walaji wanapotumia teknolojia na namna wanavyoweza kuzitatua changamoto hizo.


Hayo ameyasema leo Mei 30 jijini Dar es salaam na  ,Mwenyekiti wa Tume ya  Ushindani (FCC), Dkt Aggrey Mlimuka wakati kuhitimisha kongamano la  kuadhimisha siku za Haki za Mlaji linalo fanyika kila tarehe 15 machi duniani linakiwa  na kauli mbiu ya 'Matumizi ya Akili mnemba yanayozingatia Haki na Uwajibikaji kwa Mlaji.


"Ni wakati mzuri  sasa mamlaka za usimamizi wa soko ikiwema FCC na mamlaka nyingine zinazosimamia  mifumo ya teknolojia kukaa pamoja na kujadili ili kuja na mapendekezo ya namna bora zaidi ya matumizi ya akili mnemba kwa walaji"amsema mlimuka

Ameongeza kuwa matumizi ya akili mnemba katika huduma za malaji yabainishwe faida na athari  hasi ili kuwezesha watunga sera, sheria, mifumo ya usimamizi  na uthibiti pamoja na watafiti kuthibitisha faida n  hasara zilizopo.

"Walaji wana hofu namna ya mifumo huduma inayotumia akili mnemba namna inavyoundwa"amesema


Aidha amesema wote wanashauku ya kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa ubora zaidi kwa walaji kwa kutumia teknolojia kama vyenzo muhimu kwa ustawi wa maslahi ya walaji na uchumi kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa  Tume ya ushindani, Bw William Erio, amesema kongamano hilo limekutanisha waatalumu wa mifumo kutoka sekta za benki, usafirishaji pamoja na sekta nyingine za huduma ambao wataeleza ufahamu wao wa akili mnemba na kwa namna gani itakuwa inatumika duniani na katika nchi yetu.

Amesema kuwa wadau  hao watajadili kwa pamoja kuona namna gani wataweza kutekeleza haki za mlaji katika mazingira ya matumizi ya akili mlemba na kama kutakuwa na kikwazo cha kisheria hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kupitia taratibu za kiserikali na kuhakikiha matumizi ya akili mlemba yanatumika kisheria na walaji wanalidwa.

"Fcc kama taasisi iliyopewa jukumu la kumlinda mlaji inaweza ikawa na kanuni na sheria ambazo zinazingatia kumlinda mlaji wakati matumizi yanayofanyika ni ya akili mnemba" amesema urio

"Unapofanya  huduma za kupata usafiri  kama huba zile huduma zinapofanyika ni akili  mlemba, unapokata tiketi za ndege kinachofanya kazi ni akili mnemba, tuangalia kwenye upangaji wa bei kama inafanya haki kwa mlaji"
Previous Post Next Post