AZAM TV YAZINDUA TAMTHILIA MPYA YA TOBOATOBO KUONYESHWA KUANZIA FEBRUARI 9


Na Mwandishi Wetu

Tukiwa mbioni mwisho wa Msimu wa AFCON BOMBA Azam Media LTD kupitia chaneli 103 wanakuja na tamthilia ya Toboatobo itakayoanzwa kuonyeshwa Februari 9 ,2024 kuanzia Ijumaa mpaka jumapili saa moja na nusu usiku .

Akitambulisha Tamthilia hiyo katika mkutano na Waasanii waliicheza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam Sophia Mgaza amesema Tamthilia hiyo inachukua kijiti cha tamthilia ya Kaza Moyo inayofikia tamati Februari 3 Mwaka huu hivyo wanaopenda burudani wasipitwe kwani kuna vionjo vya kutosha maisha halisi ya jamii yetu .

“Tamthilia hii iliyosheheni wasanii nguli na wale wanaochipukia imeandaliwa na Mayunga The Best Event and Peoduction Company Limited na miongoni mwa waigizaji mahiri ikiwemo Abdalah Mkumbila ( Muhogo Mchungu )Shamira Ndwangira(Big Star ) na wasanii wengine wanaofanya vizuri” amesema Mgaza

Sambamba na hayo Mgaza akielezea vionjo vya Tamthilia hiyo anasema inaanza na kifo cha Mzee toboatobo ambaye ana watoto 22 ambao walikuwa hawajuani kufuatia marehemu Toboatobo kuwa na wake wanne kwa sir huku kila mmoja akiwa hamjui mwenzake pia sintofahamu hiyo inawahusisha na michepuko wake wanne aliwaoa kwa kificho tena.

Baada ya hapo Mzee Simbakila anaamu kukaa nyumba moja na wake wa Toboa tobo pamoja na watoto wake 22 kufuatilia mienendo yao baada ya kifo cha baba yao nanai anastahili kupewa jukumu la urithi ili kusimamia mali bila kuzifuja hatua hiyo inasababisha visa mikasa ya kufurahisha na kuburudisha kusisimua kuchekesha na tabia zilizoonyeshwa kwenye hiyo nyumba zinamfanya kaka wa marehemu kusalimu amri

Aidha Wasanii wameshauriwa kuendelea kutuma kazi zao kwa imeli ya azam wasipige simu ila kazi zao ziwe dakika 90 kila kipande zisimchoshe matazamaji
Previous Post Next Post