SERIKALI YATOA MAAGIZO HAYA SABA KWA TANESCO


Na Mwandishi wetu. 

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ametoa maelekezo saba kwa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), likiwemo la kuhakikisha shughuli ya kurekebisha mitambo inamalizika kwa wakati ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa nishati hiyo.

Waziri Kapinga amesema masuala mengine kuhakikisha wanazifanyia kazi kwa haraka hitilafu zote zinazotokea ili umeme uendelee kupatikana.

Ametoa maelekezo hayo leo Jumatatu Oktoba 2, 2023 alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme wa megawawati 43 unaotokana na gesi asilia cha Tegeta wilayani Kinondoni. Akisema hali ya uzalishaji wa umeme katika kituo hicho unaendelea vema.

"Pamoja na kuja kukagua kituo hiki nimewaelekeza Tanesco kuendelea kuboresha huduma kwa wateja. Watanzania wanapopata changamoto ndogo ndogo za umeme ikiwemo hitalafu wahakikishe wanazitatua kwa wakati.

"Tanesco iimarishe mfumo wake wa huduma kwa wateja, hatutakubali wananchi kulala giza kwa sababu transfoma au mita haijarekebishwa kwa wakati. Waimarishe mifumo yao na kufuatilia kwa ukaribu kuhakikisha wateja wanapata huduma bora," ameseka Kapinga.

Mbali na hilo, Kapinga amelitaka Tanesco kuunganisha huduma ya umeme maeneo yenye miundombinu kwa wakati ili Watanzania wafurahie huduma ya upatikanaji wa nishati hiyo.
Previous Post Next Post