WATANZANIA WASHAURIWA KUWA MAKINI NA MATAMSHI YA WANASIASA


Na Mwandishi Wetu,

Taasisi ya wazalendo Tanzania, wamewataka baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wakiwemo Tundu Lissu ambao wanafanya uchochezi kuzungumza mambo ya uongo kwa dhamira ya kuvunja amani na utulivu iliyopo kwani yanachochea upotevu wa amani nchini

Aidha wamesema watakwenda kuwaweka hadharani wale wote wanao wafadhili na kushirikiana nao katika dhamira hiyo ovu ya kuvunja amani ya taifa letu.

Wito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Taasisi ya wazalendo Tanzania, Frank Rugwana wakati akizungumza na waandishi wa Habari Jana Jijini Dar es Salaam kuhusu muelekeo wa nchi ya Tanzania.

"Tunawataka wakina Lissu na wenzake waache kuwachochea watanzania washindwe kuwa wamoja"

Alisema zipo njia sahihi za kushawishi watanzania wakubali kuwaunga mkono kwenye Chama chao na sio kuwapa taarifa za uwongo ili Kuhamasisha hasira na chuki kwa serikali yao.

"Tunatoa rai kwa niaba ya wananchi wazalendo na kwa maslahi mapana ya amani na ustawi wa taifa letu kuwasihi wakina lisu na makundi yote yaliyo nyuma yao kuacha mara moja kutugawa watanzania waache kuchochea chuki dhidi ya mhe rais na 
 waheshimu nakuthamini uhuru uliopo sasa wa kutumia jukwaa la siasa kistaarabu"

"serikali hii inaongoza wananchi wengi ambao hawana chama hawana upande wowote wachache wenye vyama tukishindwa kuelewana amani ikatoweka wote hatutokuwa salama wenye chama wasio na chama wenye dini na wasiokuwa na dini hivyo tupuuze maneno ya uchochezi tukemee mtu yeyote atayejaribu kuvunja amani yetu." Alisema Rugwana

Rugwana alisema wanafahamu mpango wa lisu ni kuwa raisi wa tanzania, ni ndoto nzuri lakini hatokuwa salama kama atafanikiwa katika mpango huo kwa njia anayoitumia ya kuwagawa watanzania.

Aliongeza kuwa serikali imetoa uwanja mpana kwa watanzania wote kutoa maoni yao juu ya uwekezaji wa bandari lakini kila kukicha lisu na wenzake wanatumia fursa hiyo kumchafua mhe raisi kwa makusudi ili wapate huruma ya watanzania 2025 kwenye uchaguzi mkuu
 
"lisu hana utakatifu wa kuikosoa serikali; amekuwa mbunge zaidi ya miaka10 ni mabadiliko gani ameyafanya 
jimboni kwake?
amekuwa makamu m.kiti wa chama kikubwa cha upinzani ametumiaje? hiyo fursa kuwasaidia watanzania licha ya kuizunguka dunia?
fursa gani ameileta kwa watanzania ili awashawishi anafaa kuwa raisi wa tanzani? "

"sisi tunamtaka kama amechoka kuwa mtanzania aende kule ambako ana makazi ya kudumu achukue uraia kabisa.
watanzania tunapaswa kubadilika mtu kabla hatujamchagua tumuulize amefanya nini? sio tumpe ili afanye no: hayo ni mambo ya kizamani "

Kadhalika Rugwana alisema watanzania wasukubali kumchagua mtu kwasababu ya kusema tu! bali wamkubali mtu yeyote ambaye anasema na kutenda tujielekeze zaidi kwenye vitendo sio maneno

Alisema watanzania sio utamaduni wetu kuchukiana, sio utamaduni wetu kupigana ama kukosa kuelewana, misingi ya amani tuliyokuwa nayo inajengwa na maridhiano, mshikamano, upendo umoja na kujisahihisha ndivyo amefanya Rais samia kufuta kesi za kisiasa kwa wanasiasa wote, kufungua mlango wa maridhiano, kuruhusu mikutano ya adhara, kuridhia mchakato wa katiba mpya jambo ambalo limekuwa kiu kwa wanasiasa na watanzania wengi 

Aidha Aliongeza kuwa" Rais Samia ameonesha upendo kuwa mpambanaji kuitafutia fursa inchi yetu ili tupige hatua za kiuchumi, ameonesha mshikamano kuruhusu uhuru wa maoni na ushahuri kushirikisha viongozi wa vyama vyote na wadau katika kuliongoza taifa kwa pamoja lakini pia ameonyesha upendo wa kukaa pamoja meza moja ya majadiliano kuhusu muelekeo wa inchi yetu"
Previous Post Next Post