MAMA SAMIA APEWA MAUA YAKE NA KAMPUNI YA FEMA


Na Mwandishi Wetu, Geita

KAMPUNI ya FEMA MINING AND DRILLING LTD inayojihusisha uchimbaji,uchongaji na ulipuaji wa madini nchini imeshukuru serikali ya awamu ya sita(6) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Hassan Suluhu kwa kuwapa fursa na nafasi kampuni za kizawa kufanya kazi katika migodi ya nchini.


Akizungumza hayo katika maonesho ya Madini(20-30 September mwaka 2023) yanayofanyika katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita Mfanyakazi wa FEMA MINING AND DRILLING LTD Mhandisi Jackline Mtei amesema " Napenda kumshukuru Rais Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kutengeneza Mazingira ya uwezekano wa wazawa 'makampuni mama' kuweza kufanya kazi katika migodi yetu hii ya kati pamoja na Migodi mikubwa,Kupitia kampuni yetu ya FEMA sisi ni kampuni zawa kampuni ya kitanzania kwa hiyo tumeona mama alivyotengeneza mazingira ambayo imetuwezesha kapata zabuni katika migodi ya kati na mikubwa"


Aidha,Jackline Mtei ameeleza fursa ya ajira kwa wanawake katika sekta ya madini alisema "kupitia kampuni yetu imeweza kutusaidia sisi wanawake kupata ajira zaidi ya wanawake kumi na tano wamepata ajira nikiwemo mimi"


Kwa upande wake Afisa manunuzi na usambazaji FEMA MINING AND DRILLING LTD Frank Joseph amesema "FEMA tumeweza kushirikiana na makampuni tofauti katika kuwapa zabuni katika kampuni yetu kama vile usambazaji wa vipuri,oils na virainisha kwa ajili ya mashine zetu pia huduma zingine tofauti tofauti kama za usafi,chakula na huduma nyingine za kijamii,Hivyo tumeweza kuzalisha ajira kwa kampuni zaidi ya tano"
Previous Post Next Post