KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI VIJANA UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR TUTAENDELEA KUITANGAZA NSSF



Na Humphrey Msechu, Geita 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ( Zanzibar ) Mhe. Fatma Hamad Rajab amesema ataendelea kushirikiana bega Kwa bega na Mifuko ili kuhakikisha wanaitangaza NSSF maeneo yote kama ambavyo waliweza kufanya kisiwani Pemba nahatimaye kupata wateja wengi.

Akizungumza Jana wakati akitembelea banda la Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) kwenye Maneesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini Geita Mwaka huu 2023 iliyoambatana na kaulinmbiu isemayo " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira"


Fatma amesema ataendelea kushirikiana bega kwa bega na Mfuko wa NSSF Kwa lengo la kuwapatia wateja wengi zaidi na huku akiwaapongeza watumishi wa mfuko wa hifadhi za jamii ( NSSF ) Mkoa wa Geita chini ya Meneja wake Winniel Lusingu kwa uwajibikaji wao katika kuwatumikia wateja wao.

" Nitashirikiana nanyi bega kwa bega ili kuhakikisha NSSF inapata wateja wengi zaidi kama ambavyo waliweza kufanikiwa kisiwani Pemba na tukapata wateja wengi zaidi ambao sasa hivi wanakwenda Dar es salaam au Tanzania kutafuta nyumba na Viwanja, lakini pia nitahakikisha watu wengi wanajiunga na Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) hadi kieleweke" amesema Fatma.


Aidha aliwapongeza watumishi hao kwa kufanya kazi kwa umoja, mshikamano na upendo, hakika mnapiga kazi nzuri sana, na kinachosababisha ni umoja wao na hivyo kuwataka kuendelea kuwa wamoja, lakini pia amewataka watumishi hao kuhakikisha wanampa nguvu Mkurugenzi wao ili aweze kufanya kazi nzuri zaidi na zaidi ili kuhakikisha NSSF inaendelea kufanya vizuri.

" Lakini pia muwe karibu sana maana mie anasema yeye ni lulu,lakini mie nasema yeye ni dhabhabu, hivyo hiyo Dhahabu muwe nayo karibu sana ili kuhakikisha kazi zote zinakwenda vizuri,lakini mnasaidiana katika matukio yote ikiwa ya kazi, ikiwa ya kijamii hakikisheni mnashirikiana ili kuhakikisha wote mnafanya kazi kama timu ya pamoja" amesema Katibu Mkuu Fatma.


Aidha Meneja wa Mfuko wa hifadhi ya jamii ( NSSF ) Mkoa wa Geita Winniel Lusingu amesema Mfuko huo unaangalia Sekta binafsi na Sekta isiyo rasmi, hivyo kuwepo kwenye Maonyesho hayo wako kwa wadau wao muhimu .


" Kuwepo hapa kwenye Maonyesho haya kwakweli ni wadau wetu ambao wanatusaidia kwa kiasi kikubwa sana cha mchango, kwani Ofisi ninkama imehamia hapa , wanacha wakija hapa wanapata huduma zote kama wako Ofisini, lakini kwasababu NSSF tumeenda mbali zaidi Kiiteknolojia tunahakikisha kwamba wanachama wetu popote wanapo kuwepo wanaweza kupata huduma za NSSF kikamilifu na kwaurahisi zaidi" amesema Winniel Lusingu.
Previous Post Next Post