TANZANIA INAJIMARISHA KATIKA KUPAMABANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO


Na Humphrey Msechu,

Serikali ikishirikiana na wadau mbali mbali katika kufanya tathmini ya utayari wa kupambana na magonjwa ya milipuko na kuambukiza ili kuhakikisha wanapata mpango mkakati wa utekelzaji ambao utawezesha kulinda afya za wananchi 


Akizungumza katika washa hiyo agosti 14, 2023 jijini Dar es salaam Mkurugenzi Msaidizi idara ya ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa idara ya kinga Wizara ya Afya Vida Mbaga 
Amesema kuwa lengo ni kufanya zoezi la kujipima utayari wa Nchi katika kuthibiti majanga na magonjwa ya milipuko yanayosabisha watu kuuguwa na vifo 


Aidha Wizara ya Afya chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu inashirikiana na vyuo, taasisi na sekta mbalimbali katika kudhibiti magonjwa na majanga “ Leo tupo hapa na wadau kutoka nje ya Nchi linakuwa ni zoezi shirikishi la kujipima kwa pamoja ili kuiangalia mapungufu na kuteengeneza mpango wa kuthibit, kujikinga na kuzuia magonjwa mlipuko majanga mengi yanayoathiri afya” amesema Mbaga 


Hata hivyo Afisa afya kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na dharura za kiafya TAMISEMI amesema baada ya kukamilika mpango mkakati wa kudhibiti ndipo Ofisi ya Rais TAMISEMI itachukua hatua ya utekelezaji
Previous Post Next Post