JESHI POLISI KANDA MAALUM TARIME RORYA LAFURAHISHWA NA MATOKEO CHANYA YA IAWP



Na ASP MINJA, Habari Tarime Rorya.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Tarime Rorya limefurahishwa na matokeo chanya ya maofisa wake walioshiriki Mkutano wa Nne wa Mafunzo wa Jumuiya ya askari Polisi wa kike Duniani (IAWP) kanda ya Afrika 2023 mwisho mwa Mwezi Julai mwaka huu Jijini Dar es salaam.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa TPF-net Kanda maalum Tarime Rorya Mrakibu Mwandamizi wa Polisi SSP Mbunja Matibu ambapo amesema askari wameonyesha kwa vitendo namna ya kutanzua uhalifu hususani ule unaovuka mipaka.


SSP Matibu amebainisha kuwa askari hao wajifunza namna ya kukabiliana na uhalifu huo pamoja na kughushi nyaraka na ushiriki wa askari wa kike katika kulinda amani kwenye mataifa yenye changamoto za kiusalama.


Ameeleza kuwa askari hao tangu walipo hitimisha mafunzo yao wameonyesha mabadiliko katika kupambana na uhalifu unaovuka mpaka huku akibainisha kuwa Mkoa huo ni mmoja ya mikoa ya Mipakani mwa Nchi ambapo askari hao wamekuwa wakitoa huduma katika maeneo hayo.


Sambamba na hilo wajumbe hao wamehimizwa kuwa mabalozi wazuri katika maeneo wanakofanyia kazi na kuwaelekeza askari wenzao yale waliyofundishwa ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Katika mkutano huo jumla ya wajumbe 40 kutoka Wilaya zote sita za Mkoa wa Tarime walihudhuria na kupata mafunzo hayo.




Previous Post Next Post