VIJANA WAASWA KUTUMIA FURSA WANAZOPATA KUTOKANA NA UJUZI WALIONAO


Na Mwandishi Wetu

Serikali imewataka vijana kutumia fursa wanazopata kutokana na ujuzi tuu walipata hususan wale wanaopewa mafunzo maalumu kwenye program zinazotolewa na kusimamiwa na Wizara ya Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu.


Hayo yamesema na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Patronasi Katambi alipotembelea Chuo cha Ufundi cha Vikindu Catholic Polytechnic kilichopo Vikindu Mkoa wa Pwani.


Akiwa chuoni hapo, Naibu Waziri Katambi alipata fursa ya kutembelea katika karakata mbali mbali ilikujionea vitu ambavyo wanafunzi wanavifanya kutokana na ufadhili wanaopata wa Serikali.


Chuo hicho cha Vikindu Catholic Polytechnic kinajumla ya wanafunzi 392 walichaguliwa kuanza mafunzo, waliodailiwa kwa  mafunzo haya walikuwa 375. Wahitimu 305 sawa na asilimia 81 ya wadailiwa; kati yao wa jinsia ya kiume walikuwa 173 sawa na asilimia 57 na wa jinsia ya kike walikuwa 131 sawa na asilimia 43. Utofauti huu ni kutokana na utoro na changamoto za kifamilia na 
kiuchumi.




Previous Post Next Post