SERIKALI KUBORESHA BOMBA LA MAFUTA TANZANIA-ZAMBIA


Na Mwandishi wetu,

SERIKALI kupitia wizara ya nishati imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanzania kwenda Zambia ili kuliwezesha bomba hilo kuwa na tija iliyokusudiwa katika kukuza uchumi wa nchi.


Akizungumza na waandishi wa habari  jijini dar es salaam waziri wa nishati, January Makamba amesema serikali inatarajia kufanya maboresho ya bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,710 ili kuliongezea ufanisi hali itakayosaidia kupunguza gharama za mafuta na vilevile kusaidia mikoa ya kusini mwa tanzania kupata mafuta kwa gharama nafuu zaidi 

Vilevile amesema uborehwaji wa bomba hilo linalosafirisha lita milioni 90 za mafuta ya dizeli kwa mwezi kutasaidia kuongeza kiasi cha mafuta kinachosafirishwq na bomba hilo lakini pia kuliwezesha kusafirisha bidhaa nyingine zaidi.


Katika hatua nyingine Mhe Makamaba amesema ujenzi wa bwawa la kufua umeme la nyerere lenye lita za ujazo bilioni 30 umefikia asilimia 89 ambapo kukamilika kwake kutaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.
Previous Post Next Post