MUHAS YAWA NAFASI YA TATU KWA UBORA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA


Na mwandishi wetu,

Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimekuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu vitatu bora katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa kimataifa wa Times Higher Education (THE)


Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 11, 2023 jijini Dar es salaam Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Prof. Appolinary Kamuhabwa amesema ripoti imebaini kuwa MUHAS ni taasisi ya tatu kwa ubora kati ya taasisi 121 ambapo nafasi ya kwanza imeshikwa na Chuo Kikuu Cha Witwatersrand na nafasi ya pili Chuo Kikuu cha Johannesburg vyote kutoka Afrika ya kusini 


Miongoni mwa vigezo muhim vilivyoangalia katika ripoti hiyo ni ufundishwaji, kipato cha taasisi na tafiti zilizofanyika na taasisi 


Aidha nafasi hi itambulisha Nchi kimataifa, itaweza kuleta ongezeko kubwa la wanafunzi wakimataifa kutuko nchi mbalimbali kwa kuzingatia viwango vya ubora iliyonayo pamoja na hayo taasisi itaweza kupokea fedha za tafiti, na wanafunzi wano hitimu kupata soko la ajira ndani na nje ya Nchi.
Previous Post Next Post