MSAMA AWASHAURI VIONGOZI MBALIMBALI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA KWA JITIHADA ANAZOFANYA


Na mwandishi wetu
Viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge, wameshauriwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa.

Akizungumza mapema leo,Julai 6, 2023, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema kuwa Wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania, na kwamba, hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais.


“Watu wote ambao wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha Amani, Utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo.

“Rais anafanya kazi kubwa sana, mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu, haya yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye Nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha Biashara ili kukuza uchumi wa nchi” amesema.

Previous Post Next Post