TRA YAPOKEA MAONI YA WADAU WA SEKTA YA UTALII KWENYE MAONESHO YA KARIBU KILL FAIR


Na Mwandishi Wetu, Arusha

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imebainisha kuwa, ipo katika kupokea maoni ya wadau wa sekta ya utalii katika masuala ya utozaji wa kodi ili kuimalisha uchumi wa nchi kwani sekta hiyo ni sekta muhimu hapa nchini.
 
Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa kodi, Richard Kayombo amebainisha hayo Jijini hapa katika maonesho ya Utalii ya Karibu Kill Fair yaliyoanza leo Juni 2-4, mwaka huu katika viwanja vya Magereza, Kisongo Arusha.

‘’TRA  kwa kushirikiana na Mameneja wetu wa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Meneja wa Arusha, Kilimanjaro, Manyara pamoja na Meneja wa Tanga, tupo hapa kwa lengo kuu la kushirikiana na wadau wetu wa sekta ya Utalii
Kwa lengo la kushirikiana kwa namna mbalimbali ikiwemo kueleweshana na wahusika kulipa kodi kwa wakati na kwa utaratibu wa kisheria’’ amesema Kayombo.
 


Ameongeza kuwa, wanapokea maoni ya wadau hao wa sekta ya Utalii kwani imekuwa ni miongoni mwa sekta kubwa inayobeba sektta nyingi ndani yake hivyo wanaamini Nchi ikishindwa kukusanya mpato yake vizuri, nchi itakosa miundombinu mizuri na watalii watashindwa kutembelea hivyo wanatoa elimu sahihi na kupokea maoni kuona namna bora ya ulipaji kodi.

‘’Tunatambua sekta ya utalii, inagusa sekta ya anga, usafiri wa ardhini, hoteli, matumizi ya mafuta, na matumizi mengine, hivyo tunatambua Utalii ukiwa imara, na sekta zingine zote zitasimama imara, ila sekta ya utalii ikiporomoka zingine zitaumia na Serikali itakosa mapato.

Serikali ikikosa fursa ya mapato na miundombinu itakosa kujengwa na maeneo mengine itakosa fursa kutokana na kutofikiwa kwa watalii.’’ Amesema Kayombo.
 

Kayombo ameongeza kuwa, wanatumia maonesho hayo kwa siku zote za maonesho na huduma zingine zitaendelea ikiwemo Elimu ya kwa mlipa kodi.
  
Aidha, Amesema kuwa, utalii kanda ya kaskazini ni mwakilishi wa utalii kanda zote za Tanzania Bara, huku pia utalii ukiwa katika Visiwa vya Zanzibar. 


Previous Post Next Post