DOLSON INTERIORS YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA.
 
Kampuni ya Dolson Interiors inayofanya bidhaa za ndani za ubunifu yaipongeza Serikali ya awamu ya sekta kwa kuweka mazingira wezeshi katika sekta ya viwanda nchini.
 
Hayo yamesemwa na  mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo, Victoria  Martin  katika maonesho ya Nne ya Karibu Kill Fair2023 yanayofanyika Jijini hapa, kwenye viwanja vya Magereza Kisongo
 

Amesema; ‘’Sera wezeshi ya uwekezaji chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan, Dolson wameweza kuja na teknolojia ya bidhaa mbalimbali ikiwemo magodoro, masofa, mapazia na mazuria kuwafikia wateja mbalimbali ikiwemo sekta ya Utalii.
 


Amesema kulingana na soko la ushindani wa kibiashara,  wao wamejikita zaidi kuwahudumia wadau wa hoteli, taasisi za kifedha, makapuni binafsi  na wengine wengi.  
 

Kwa upande wake, Salim Idrisa ambaye ni mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo amesema kuwa, wapo kushiriki kwenye maonesho hayo ya Karibu Kill Fair katika kutangaza zaidi biashara yao hiyo ambayo sasa ni takribani miaka 18 iliyopita ambapo amesema ubora wa kazi zao ndio zinazowapa fursa za kuendelea kuendelea kufanya kazi za ubora zaidi.

 

Previous Post Next Post